Saratani sio ugonjwa wa kisasa - BBC

Ugunduzi huu ni muhimu katika kusaidia watafiti kubaini chanzo cha Saratani
Watafiti nchini Uingereza wamegundua kuwepo Saratani katika mifupa ya kijana mmoja aliyeishi nchini Misri miaka elfu tatu iliyopita.
Hii ni miaka elfu mbili kabla ya kisa cha kwanza cha ugonjwa huo kuthibitishwa.
Mtafiti Michaela Binder, aligundua kuwa mifupa hiyo, ilikuwa na mashimo, na kugundua kuwepo aina ya Saratani katika mifupa hiyo.
Ugunduzi huu unaonyesha kuwa Saratani sio ugonjwa wa kisasa tu na hivyo wanasayansi watapata kuchunguza ambavyo ugonjwa huu ulianza miaka zaidi ya elfu moja iliyopita.

Post a Comment

أحدث أقدم