Ng’ombe
150 wameuawa na askari wa Wanyama Pori katika Hifadhi ya Biharamulo, kutokana
na mgogoro uliokuwepo wa kuwaondoa baadhi ya wafugaji, waliovamia eneo la
hifadhi.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, amekiri kuuawa
kwa ng'ombe hao wakati akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana.
Alisema
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda amewaagiza baadhi ya mawaziri kwenda wilayani humo,
kusuluhisha mgogoro huo, na kwamba kwa sasa wamefikia mahali pazuri.
"Tuko
huku baadhi ya mawaziri, tumeagizwa na Serikali Kuu kuja kushughulikia mgogoro
huu, kulikuwa na mgogoro ambapo watu waliokuwa wakiondolewa hifadhini, sasa
mchakato huo ukasababisha ng'ombe hao uliowataja kufa," alisema Waziri
Tibaijuka.
Alisema
wachungaji wa ng’ombe hao, walikamatwa ndani ya hifadhi pamoja na mifugo
yao, na utaratibu ulipaswa kuwapiga faini au kufikishwa mahakamani
kwa wale watakaogoma kulipa faini, lakini katika mazingira hayo kuliibuka
mgogoro huo.
"Tuko
huku na sasa hivi ndiyo tumetoka kwenye kikao cha kushughulikia mgogoro huu,
lakini mpaka sasa tumeshafikia pazuri," alisema Waziri Tibaijuka.
إرسال تعليق