UCHAGUZI SIMBA SC NJIANI KUANZA BAADA YA SERIKALI KUKABIDHI KATIBA .


_DSC0696 
KATIBA ya Wekundu wa msimbazi Simba sc  imekamilika baada ya kufanyiwa marekebisho na kukabidhiwa  kwa uongozi wa klabu hiyo chini ya mwenyekiti Ismail Aden Rage.
Katibu mkuu wa Simba sc,  Ezekiel Kamwaga amezungumza na waandishi wa habari leo hii na kueleza kuwa tayari wameshakabidhiwa katiba yao kutoka serikalini na kinachofuata na kuanza kwa mchakato wa uchaguzi .
Awali uchaguzi wa Simba ulitakiwa kufanyika wiki iliyopita, lakini kutokamilika kwa katiba kulikwamisha mchakato mzima.
Kamwaga alisema baada ya zoezi la katiba kukamilika, kesho wanatarajia kukutana na kamati ya uchaguzi chini ya mwenyikiti wake, Mwanasheria Dkt. Damas Ndumbaro  ili kupanga mchakato mzima.
Katibu huyo aliongeza kuwa  baada ya kamati kukutana, taratibu zote zitawekwa wazi na wenye nia ya kugombea wataanza rasmi mchakato.

Post a Comment

Previous Post Next Post