Kamishna
wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, amethibitisha
kuwa Jeshi lake limefanikiwa kumkamata jambazi sugu aitwaye Paulo Thamas
Milanzi maarufu Chinga (35), Mmakonde mkazi wa Chanika.
Amesema
baada ya majibizano ya risasi jambazi hilo lilijeruhiwa na kufikishwa
hospitali ya Muhimbili kwa matibabu lakini baadaye alifariki dunia.
Alisema jambazi huyo lilikuwa akitafutwa na polisi
kutokana
kuhusika kwenye matukio ya mauaji na wizi ikiwemo tukio la kuuawa kwa
Afisa Mwandamizi wa Usalama wa Taifa, Sylivabus Adrian Mzeru Aprili 29,
2014 liliotokea Uwanja wa Ndege.
Aliongeza kuwa Chinga alikamatwa na bastola aina ya Star.'
Majambazi wenzake walikamatwa na kwa sasa wako gerezani wakisubiri taratibu za kisheria kuchukua mkondo wake.
إرسال تعليق