Taarifa
ya ndani ya Oktoba 2, mwaka huu ya Kikosi cha Usalama Barabarani Makao
Makuu Dar es Salaam iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, imesema
askari hao walisimamisha gari dogo na baada ya dereva kujitetea,
waliendelea kutafuta makosa hali iliyosababisha abiria aliyekuwa
mgonjwa kufariki.
Kutokana
na tukio hilo, makamanda wa polisi wa wilaya zote za Mkoa wa Kipolisi
wa Dar es Salaam wametakiwa kuwakumbusha askari wao kuepuka
kutolazimisha kutafuta makosa ambayo hayana madhara.
“Makosa
ambayo hayana madhara katika kusababisha ajali mfano ni vifaa vya
kuzimia moto, rangi, kadi kutoandika anuani, motor vehicle, leseni
chini ya siku 30 na kadhalika,” lilisomeka agizo hilo kwa makamanda hao wa polisi.
إرسال تعليق