PILIPILI
Entertainment wanaonekana kutaka kuleta mapinduzi ya sinema za Tanzania kwa
kuanza kuleta sinema ambazo zinazungumza kiswahili kinachoeleweka miongoni mwa
filamu bora duniani.
Ingawa imeelezwa mahali kwamba ni sinema ya pili ukianzia na ile ya Jimmy, mimi nataka kuzungumzia filamu hii ya Mzimu ambayo kwa kidosi inaitwa Bhoot.
Filamu hii ya mwaka 2003 iliyochezwa na Ajay Devgan na Urmila Matondkar na kuongozwa na Ram Gopal Varma na pia kutayarishwa pia kwa lugha ya Telugu kama 12 Va Anthasthu ndio sasa imeletwa nchini Tanzania kwa Kiswahili na kupewa jina Mzimu na majina ya washiriki wa kimazingira yamebadilishwa na kuwa ya Kiswahili zaidi.
Ni moja ya filamu za kidosi zilizotengenezwa kwa mwelekeo kidogo tofauti za kawaida za filamu zenye muziki wa dansi na kudansi ingawa vifereji vyake takaribani sana vilikuwa vya kidosi.
Wakati ilipotengenezwa mwaka 2003 ilimeza watu na kufanya vyema katika chati za sinema za Bollywood na huku Urmila akitwaa tuzo nyingi kwa kucheza kama mke aliyeingiwa na mzimu wa mtu aliyeuawa kwa hila baada ya kumkatalia penzi.
Ukitazama sinema ya Kiswahili (nilibahatika kuona ya Kiingereza) utaona wazi kwamba binti huyu Urmila Matondkar ndiye hasa aliyetawala sinema hii, toka inaanza mpaka mwisho.
Ni raha sana kuona jinsi midomo inavyocheza kama vile wanazungumza Kiswahili wakati kiukweli asili yake ni maongezi ya Kingereza au Kihindi.
Ukimwangalia mwanadada yule miaka hiyo alivyocheza kwa makini hutasita kumpa asilimia 100 mtu ambaye aliingiza maneno ya Kiswahili katika mdomo na pia fundi aliyecheza nayo mpaka ikaonekana kwamba Yule mtu anazungumza Kiswahili.
Sinema hii ya Mzimu katika uasili wake ina namba mbili inayoitwa Bhoot Returns iliyotoka Oktoba 12, 2012 na ni matumaini yangu kwamba itamaliziwa na hii ili kutoa ladha mpya katika sinema za Kiswahili duniani.

Tuzungumzie simulizi lake
Simulizi lake ni la Vishal (Ajay Devgn) ambaye
amemuoa Swati (Urmila
Matondkar). Wawili hao wananunua flati kwenda kuishi lakini kwa bei
ambayo inashangaza sana.
Watu hawa hawakushtukia dili hilo
lakini mwenye eneo(anayeliangalia) Bw
Thakkar (Amar Talwar) anamweleza kwamba mjane mmoja Amandeep Singh (Barkha Madan),alikuwa
anaishi hapo lakini kwa bahati mbaya alijiua baada ya kumuua mtoto wake.
Vishal hakumwambia mkewe ukweli huo,
kwani anaficha ukweli huo kwani kwa
namna yoyote Swati asingelikubali lakini
kwa bahati mbaya katika simulizi unabaini kwamba Bw.Thakkar yanamtoka na swati
anajua lakini akiwa ndani na mzimu nao unaanza kusumbua.
Swati hapendi hali hiyo na
anazungumza na Vishal, ingawa yeye mwenyewe hakuamini mambo ya mzimu. Lakini
siku zinavyoenda vishindo vinavyotokea mle ndani vinatisha hasa baada ya Swati
kuanza kuingiwa na mzimu huyo anayedaiwa kujiua.
Mambo yanapoharibika Vishal
anatafuta msaada kutoka kwa daktari Rajan (Victor Banerjee). Lakini
baada ya kuanza kuangalia tatizo hilo Vishal
na mtoto wa Thakkar, Sanjay (Fardeen
Khan) wanashuhudia Swati akimuua kwa namna ya ajabu mlinzi wa jengo
lile.
Sanjay ambaye alifika pale kumuona
baba yake alishuhudia na kuamua kumweleza inspketa Qureshi(Nana Patekar), nini
kilichojiri na kuanza kuwa na mashaka na wawili hao.
Baadae msaidizi nyumbani kwa Vishal
anamsaidia kumwelimisha na yeye kuamua kumfuata mganga wa kienyeji Sarita (Rekha) ili kusaidia kukabiliana na Mzimu
huo.
Sarita anaona mzimu wa Aman na mtoto
wake.
Mganga huyo anamshauri Vishal
kukutana na mama yake Aman (Tanuja),
kwani ndiye anaweza kuzungumza na mzimu wa binti yake.
Vishal anamtafuta mama yake Aman na
kupata maarifa zaidi kuhusu binti yule na kukubali kwenda naye.
Na wakiwa hapa walimtega Sanyay
ambaye alikanusha kujua chochote kuhusu Aman.
Hata hivyo anataka kuondoka na
katika patashika hizo Swati anamzuia na katika hilo kuna vitu vinafanyika na
kisha mwisho unafika ambapo Sanjay anakiri kufanya mauaji miaka mingi
iliyopita.
Sanjay anatupwa jela baada ya kukiri
na huko bado anakutana na shida nyingine.
Ukweli ulijulikana baada ya Sanjay
kubanwa kimaajabu na kujikuta akiangaliana na nondo zilizochomoza na ndipo
alipoambiwa aseme na akakiri kwamba alimuua.
Tabu kubwa ya filamu hii ni kuwa majina halisi ya
watu katika simulizi la kidosi yamebadilishwa.Humu kuna majina ya Kiswahili
kabisa kama tupo bongo , Vishal aliitwa Victor Swati alikuwa Suzy namke aliyeuawa alitambuliwa
kama Manka na Dk Rajan kama Dk Rajabu.
NB:Ilitoka mara ya kwanza Habarileo
Post a Comment