Bhoot:- Sinema ya Kidosi yenye kuzungumza Kiswahili inaitwa Mzimu

PILIPILI Entertainment wanaonekana kutaka kuleta mapinduzi ya sinema za Tanzania kwa kuanza kuleta sinema ambazo zinazungumza kiswahili kinachoeleweka miongoni mwa filamu bora duniani.
Ingawa imeelezwa mahali kwamba ni sinema ya pili ukianzia na ile ya Jimmy, mimi nataka kuzungumzia filamu hii ya Mzimu ambayo kwa kidosi inaitwa Bhoot.
Filamu hii ya mwaka 2003 iliyochezwa na Ajay Devgan na Urmila Matondkar na kuongozwa na Ram Gopal Varma na pia kutayarishwa pia kwa lugha ya Telugu kama 12 Va Anthasthu ndio sasa imeletwa nchini Tanzania kwa Kiswahili na kupewa jina Mzimu na majina ya washiriki wa kimazingira yamebadilishwa na kuwa ya Kiswahili zaidi.
Ni moja ya filamu za kidosi zilizotengenezwa kwa mwelekeo kidogo tofauti za kawaida  za filamu zenye muziki wa dansi na kudansi ingawa vifereji vyake takaribani sana vilikuwa vya kidosi.
Wakati ilipotengenezwa mwaka 2003 ilimeza watu na kufanya vyema katika chati za sinema za Bollywood na huku Urmila akitwaa tuzo nyingi kwa kucheza kama mke aliyeingiwa na mzimu wa mtu aliyeuawa kwa hila baada ya kumkatalia penzi.
Ukitazama sinema ya Kiswahili (nilibahatika kuona ya Kiingereza) utaona wazi kwamba binti huyu Urmila Matondkar ndiye hasa aliyetawala sinema hii, toka inaanza mpaka mwisho.
Ni raha sana kuona jinsi midomo inavyocheza kama vile wanazungumza Kiswahili wakati kiukweli asili yake ni maongezi ya Kingereza au Kihindi.
Ukimwangalia mwanadada yule miaka hiyo alivyocheza kwa makini hutasita kumpa asilimia 100 mtu ambaye aliingiza maneno ya Kiswahili katika mdomo na pia fundi aliyecheza nayo mpaka ikaonekana kwamba Yule mtu anazungumza Kiswahili.
Sinema hii ya Mzimu  katika uasili wake ina namba mbili inayoitwa Bhoot Returns iliyotoka Oktoba 12, 2012 na ni matumaini yangu kwamba itamaliziwa na hii ili kutoa ladha mpya katika sinema za Kiswahili duniani.
Tuzungumzie simulizi lake
Simulizi lake ni la Vishal (Ajay Devgn) ambaye amemuoa Swati (Urmila Matondkar). Wawili hao wananunua flati kwenda kuishi lakini kwa bei ambayo inashangaza sana.
Watu hawa hawakushtukia dili hilo lakini mwenye eneo(anayeliangalia)  Bw Thakkar (Amar Talwar)  anamweleza kwamba mjane mmoja Amandeep Singh (Barkha Madan),alikuwa anaishi hapo lakini kwa bahati mbaya alijiua baada ya kumuua mtoto wake.
Vishal hakumwambia mkewe ukweli huo, kwani anaficha ukweli huo kwani  kwa namna yoyote Swati asingelikubali  lakini kwa bahati mbaya katika simulizi unabaini kwamba Bw.Thakkar yanamtoka na swati anajua lakini akiwa ndani na mzimu nao unaanza kusumbua.
Swati hapendi hali hiyo na anazungumza na Vishal, ingawa yeye mwenyewe hakuamini mambo ya mzimu. Lakini siku zinavyoenda vishindo vinavyotokea mle ndani vinatisha hasa baada ya Swati kuanza kuingiwa na mzimu huyo anayedaiwa kujiua.
Mambo yanapoharibika Vishal anatafuta msaada kutoka kwa daktari Rajan (Victor Banerjee). Lakini baada ya kuanza  kuangalia tatizo hilo Vishal na mtoto wa Thakkar, Sanjay (Fardeen Khan) wanashuhudia Swati akimuua kwa namna ya ajabu mlinzi wa jengo lile.
Sanjay ambaye alifika pale kumuona baba yake alishuhudia na kuamua kumweleza inspketa Qureshi(Nana Patekar), nini kilichojiri na kuanza kuwa na mashaka na wawili hao.
Baadae msaidizi nyumbani kwa Vishal anamsaidia kumwelimisha na yeye kuamua kumfuata mganga wa kienyeji Sarita (Rekha) ili kusaidia kukabiliana na Mzimu huo.
Sarita anaona mzimu wa Aman na mtoto wake.
Mganga huyo anamshauri Vishal kukutana na mama yake Aman (Tanuja), kwani ndiye anaweza kuzungumza na mzimu wa binti yake.
Vishal anamtafuta mama yake Aman na kupata maarifa zaidi kuhusu binti yule na kukubali kwenda naye.
Na wakiwa hapa walimtega Sanyay ambaye alikanusha kujua chochote kuhusu Aman.
Hata hivyo anataka kuondoka na katika patashika hizo Swati anamzuia na katika hilo kuna vitu vinafanyika na kisha mwisho unafika ambapo Sanjay anakiri kufanya mauaji miaka mingi iliyopita.
Sanjay anatupwa jela baada ya kukiri na huko bado anakutana na shida nyingine.
Ukweli ulijulikana baada ya Sanjay kubanwa kimaajabu na kujikuta akiangaliana na nondo zilizochomoza na ndipo alipoambiwa aseme na akakiri kwamba alimuua.
Tabu kubwa ya filamu hii ni kuwa majina halisi ya watu katika simulizi la kidosi yamebadilishwa.Humu kuna majina ya Kiswahili kabisa kama tupo bongo , Vishal aliitwa Victor Swati  alikuwa Suzy namke aliyeuawa alitambuliwa kama Manka na Dk Rajan kama Dk Rajabu.
NB:Ilitoka mara ya kwanza Habarileo

Post a Comment

أحدث أقدم