Stori: Ojuku Abraham SHIRIKA
la Ndege la Fast Jet linalotoa huduma ya usafiri wa anga katika baadhi
ya mikoa ya Tanzania na nje ya nchi, limelalamikiwa na wateja wake
mbalimbali kutokana na jinsi linavyofanya kazi, Risasi Jumatano lina
habari kamili.
“Wanatangaza kuna tiketi za shilingi 32,000, ni uongo, mimi binafsi nimewahi kuulizia hizi tiketi mara kadhaa, lakini kila nikiomba ninaambiwa zimeisha na hata ndani ya ndege sijawahi kukutana na msafiri mwenye tiketi ya bei hizo,” alisema Samuel Kuntu, mkazi wa jijini Mwanza.
Aliongeza yeye amewahi kusafiri mara kadhaa na ndege za Fast Jet, lakini amegundua upungufu mkubwa wa shirika hilo, ikiwemo nauli kubwa tofauti na inavyotangazwa kwenye vyombo vya habari.
“Jana (Jumapili iliyopita) nilikuja na ndege hii na nimelipia shilingi laki nne kwa safari ya Dar, bei hii ni kubwa, nadhani ATCL ndilo shirika lenye bei rahisi, lakini si hawa,” alisema Kuntu ambaye alionekana kujua mengi kuhusu Fast Jet.
“Inapotokea abiria amechelewa ndege (no-show), Fast Jet humtaka alipe tiketi nyingine na kulipa asilimia 100, wakati mashirika mengine humtoza faini abiria ambaye amechelewa ndege kwa asilimia 25 ya bei aliyonunulia tiketi kisha kumpangia siku nyingine ya safari.
“Wakati mwingine wanaahirisha safari au ndege kuchelewa lakini mteja hafidiwi kwa chochote, ila mteja akichelewa, harudishiwi hata shilingi wala kupangiwa siku nyingine, alisema mfanyabiashara huyo anayesafiri mara kwa mara kati ya Mwanza na Dar es Salaam.
Msafiri mwingine , Sunday Shomari ambaye alisafiri na ndege hiyo akitokea Arusha kwenda Dar es Salaam, alisema alisahau simu yake ya mkononi ya gharama kubwa pamoja na Ipad yake ndani ya ndege hiyo, lakini muda mchache baada ya kurejea hakupata vitu vyake.
“Nilikuwa na mke na watoto tunatoka Arusha, tulipofika Dar es Salaam tukashuka na kuvisahau vitu hivyo kwa bahati mbaya, tulipofika nje mke wangu akaniuliza simu yako ipo wapi? Nikakumbuka nimeisahau ndani ya ndege, nikarudi uwanjani na kuwaomba walinzi wanisaidie niende nikachukue simu yangu.
Abiria mwingine aliyekataa jina lake kutajwa gazetini, alisema mshangao mwingine kwenye ndege za shirika hilo ni kuuziwa vitu ambavyo katika mashirika mengine, wasafiri hupewa bure akitolea mfano soda, bia na viburudisho vingine.
Mwandishi wa habari hizi alifika katika ofisi za Fast Jet zilizopo Barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam kwa lengo la kutaka maelezo ya uongozi kuhusu tuhuma hizo, lakini walinzi walimzuia kuingia ndani na kutakiwa kuchukua anuani ya barua pepe ya msemaji wake, kwa maelezo kwamba ndiye angeweza kumsaidia kwa mambo ya kihabari.
Mwandishi aliandika madai yote na kuyatuma kwenye anuani hiyo akitaka kuonana na uongozi kwa ajili ya kujibu maswali kadhaa, lakini afisa uhusiano aliyejibu ujumbe huo, Lucy Mbogoro, baadaye alilitaka gazeti hili kuandika maswali hayo na kuyatuma, sambamba na nakala ya sura ya mbele ya gazeti.
Lakini hata baada ya kutuma maswali hayo kama ilivyotakiwa, Fasjet wameshindwa kutoa majibu na Lucy alipopigiwa simu na kuulizwa, alidai anayehusika na majibu hayo ametingwa na kazi.
Hata hivyo, gazeti hili bado linafuatilia kwa karibu ili kupata majibu ya maswali hayo.
Wafanyakazi wa Shirika la ndege la Fast Jet.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili, baadhi ya wateja hao
wamesema kuwa, matangazo ya kila siku kuwa shirika hilo linatoa huduma
ya usafiri wa anga kwa bei nafuu ni usanii, kwani tiketi zinazouzwa kwa
bei hizo ndogo, daima huelezwa kuwa zimekwisha.“Wanatangaza kuna tiketi za shilingi 32,000, ni uongo, mimi binafsi nimewahi kuulizia hizi tiketi mara kadhaa, lakini kila nikiomba ninaambiwa zimeisha na hata ndani ya ndege sijawahi kukutana na msafiri mwenye tiketi ya bei hizo,” alisema Samuel Kuntu, mkazi wa jijini Mwanza.
Aliongeza yeye amewahi kusafiri mara kadhaa na ndege za Fast Jet, lakini amegundua upungufu mkubwa wa shirika hilo, ikiwemo nauli kubwa tofauti na inavyotangazwa kwenye vyombo vya habari.
“Jana (Jumapili iliyopita) nilikuja na ndege hii na nimelipia shilingi laki nne kwa safari ya Dar, bei hii ni kubwa, nadhani ATCL ndilo shirika lenye bei rahisi, lakini si hawa,” alisema Kuntu ambaye alionekana kujua mengi kuhusu Fast Jet.
Abiria wakishuka kutoka kwenye ndege ya Fast Jet.
Alisema shirika hilo la ndege lina utaratibu unaomuumiza mteja hasa
pale anapoahirisha safari au kuchelewa ndege, tofauti na mashirika
mengine kama Precision Air na Air Tanzania.“Inapotokea abiria amechelewa ndege (no-show), Fast Jet humtaka alipe tiketi nyingine na kulipa asilimia 100, wakati mashirika mengine humtoza faini abiria ambaye amechelewa ndege kwa asilimia 25 ya bei aliyonunulia tiketi kisha kumpangia siku nyingine ya safari.
“Wakati mwingine wanaahirisha safari au ndege kuchelewa lakini mteja hafidiwi kwa chochote, ila mteja akichelewa, harudishiwi hata shilingi wala kupangiwa siku nyingine, alisema mfanyabiashara huyo anayesafiri mara kwa mara kati ya Mwanza na Dar es Salaam.
Msafiri mwingine , Sunday Shomari ambaye alisafiri na ndege hiyo akitokea Arusha kwenda Dar es Salaam, alisema alisahau simu yake ya mkononi ya gharama kubwa pamoja na Ipad yake ndani ya ndege hiyo, lakini muda mchache baada ya kurejea hakupata vitu vyake.
“Nilikuwa na mke na watoto tunatoka Arusha, tulipofika Dar es Salaam tukashuka na kuvisahau vitu hivyo kwa bahati mbaya, tulipofika nje mke wangu akaniuliza simu yako ipo wapi? Nikakumbuka nimeisahau ndani ya ndege, nikarudi uwanjani na kuwaomba walinzi wanisaidie niende nikachukue simu yangu.
Marubani wa ndege ya Fast Jet wakiwa mzigoni.
“Wakaniambia wao hawana mamlaka ya kuingia ndani ya ndege ile, badala
yake wakanisaidia kuwaambia wafanyakazi wa ndege kuwa waniangalizie
vitu vyangu pale nilipokaa, lakini jambo la ajabu eti wakadai
hawakuviona, wakati mimi nilikuwa msafiri wa mwisho kushuka kwenye
ndege, ina maana hakukuwa na mwingine baada ya mimi kushuka ambaye
ningeweza kusema l ndiye aliyechukua vile vitu,” alisema Shomari ambaye
ni mtangazaji wa zamani wa ITV na Radio One, kwa sasa anafanya kazi
Sauti ya Amerika (Voa) jijini Washington, Marekani.Abiria mwingine aliyekataa jina lake kutajwa gazetini, alisema mshangao mwingine kwenye ndege za shirika hilo ni kuuziwa vitu ambavyo katika mashirika mengine, wasafiri hupewa bure akitolea mfano soda, bia na viburudisho vingine.

إرسال تعليق