HII NDIO KAMBI YA SIMBA JIJINI DAR HII HAPA, KAGUA MAZINGIRA

Pamoja na viongozi wa Simba kufanya siri kubwa, kikosi chao kimejichimbia kwenye Hoteli ya Kitalii ya Golden Tulip.
Simba imewasili jana usiku ikitokea Afrika Kusini na moja kwa moja kuweka kambi hiyo Golden Tulip, Masaki jijini Dar es Salaam.
Hoteli hiyo iko ufukweni mwa Bahari ya Hindi na wachezaji wake watakuwa wakitoka na kwenda kufanya mazoezi kabla ya kurejea hotelini hapo.
Kabla ya kuingia kambini hapo, Simba ilikuwa nchini Afrika Kusini ilipoweka kambi na kucheza mechi tatu za kirafiki na matokeo ni sare moja na kupoteza mbili.
Pitia picha mwenyewe uonge mazingira ya hoteli hiyo ambayo Mnyama amejichimbia...

Post a Comment

أحدث أقدم