Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Mwenyekiti wa
Kamati hiyo, Zitto Kabwe kutakuwa na mjadala wa taarifa za kifedha za
taasisi za Serikali Kuu na mashirika ya umma kuanzia Jumatatu ijayo.
Moja ya mambo yatakayojadiliwa ni madeni ya Serikali kwa Mifuko ya Hifadhi za Jamii.
Imeelezwa kuwa kamati hiyo itajigawa katika
makundi mawili, moja litashughulika na taasisi za Serikali Kuu wakati
jingine likijikita katika mashirika ya umma.
“Kundi la kwanza linaloongozwa na Zitto
litashughulikia Hesabu za Serikali Kuu na BoT na kundi la pili
linaloongozwa na Makamu Mwenyekiti wa PAC, Deo Filikunjombe
litashughulikia Hesabu za Mashirika ya Umma,” ilisomeka sehemu ya ratiba
hiyo.
إرسال تعليق