KIMBUNGA CHAUA 6 NCHINI INDIA

Upepo mkali ukivuma leo katika ufukwe wa Gopalpur huko Orissa, India.

Taswira kutoka katika Hoteli ya Park iliyopo Visakhapatnam wakati kimbunga hicho kikipita.
WATU sita wamepoteza maisha nchini India baada ya kimbunga kiitwacho Hudhud kupiga eneo la pwani ya India kikiwa na upepo unaovuma kwa kasi ya hadi kilomita 180 kwa saa.
Watu 350,000 waeondolewa kutoka maeneo ya Andhra Pradesh na Orissa wakati vituo vya huduma za dharura vikifunguliwa huku vikosi vya usalama vikiwekwa kwenye hali ya tahadhari.
Katika ripoti iliyotolewa hivi karibuni ya Idara ya hali ya hewa nchini India imeeleza kuwa hali katika eneo la baharini itakuwa mbaya katika eneo la kazkazini mwa Andhra Pradesh na katika pwani ya Orissa.
Kimbunga kikali mnamo mwaka 1999 kiliua watu 10,000 katika eneo la Orissa.

Post a Comment

أحدث أقدم