MWALIMU mmoja mkazi wa Mlole Manisapaa ya Kigoma Ujiji amefariki
dunia baada ya kugongwa na gari aina ya Hiace yenye namba CMS 688
inayofanya safari zake Kigoma mjini kwenda Kijiji cha Simbo wilayani
humo.
Akizungumzia tukio hilo, Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Lindi,
Kamishna Msaidizi (ACP), Michael Deleli, alisema ajali hiyo ilitokea
jana majira ya saa 2:00 asubuhi na kumtaja aliyefariki kuwa ni Godness
Masuruli (30), aliyekufa papo hapo baada ya kugongwa na gari hilo
lililokuwa likiendeshwa na John Makosa (34).
Alisema kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa kabla ya kukabidhiwa kwa
ndugu zake huku dereva akiwa mahabusu na atafikishwa mahakamani kujibu
mashitaka yake.
إرسال تعليق