Meneja wa T.I. na CEO wa Grand Hustle Records, Jason Geter
amesema ili msanii wa Afrika aweze kupata collabo na msanii mkubwa wa
Marekani, anahitajika kuwa na ushawishi katika sehemu anayokotoka ili
awe na kitu cha kumuongezea pia msanii huyo anayetaka kumshirikisha.
Jason Geter
Akiongea kwenye warsha iliyoandaliwa maalumu kwaajili ya wadau wa
muziki nchini Ijumaa hii, Geter alitolea mfano wa jinsi T.I.
alivyokubali kufanya wimbo na P-Square. Alisema alipigiwa simu na rafiki
yake aliyemueleza kuwa kundi la P-Square lingetaka kumshirikisha T.I.
kwenye wimbo wake lakini bahati mbaya hakuwahi kuwasikia wasanii hao.
“Kiukweli nilikuwa sijawahi kuwasikia kabla, kwasababu Marekani
hawachezwi kivile, nina uhakika baadhi ya watu wanawafahamu lakini watu
wengi Marekani hawawafahamu kabisa P-Square,” alisema.
Geter alidai baada ya kuambiwa hivyo aliamua kufanya utafiti wake
mwenyewe ili kuwafahamu wasanii hao na hivyo aliingia Youtube
kuwatazama. “Nilipoenda kufanya utafiti wangu, nikasema wow, hawa jamaa
ni wakubwa,” aliongeza.
Alidai baada ya kuona ukubwa wake, aliona kuwa P-Square wana kitu cha kumuongeza T.I.
“Sababu mashabiki wengi wa P-Square wanaweza kuwa hawajawahi hata
kumsikia T.I. Kwahiyo hicho ndio kitu cha kwanza kwamba utaenda
kumuongezea nini msanii wangu. Msanii wangu ana msingi wa Marekani
kukupa, wewe utaweza kumtambulisha kwa kitu kingine?”
Aliongeza kuwa hatua ya pili inahusisha masuala ya fedha na biashara
ambapo huusikiliza wimbo anaotaka kushirikishwa msanii huyo. Alisisitiza
kuwa mara nyingi suala la fedha au malipo ya collabo sio kitu
wanachokiweka mbele zaidi ya kuzingatia kuwa ni nini msanii wake
atakipata kutokana na kushirikishwa kwenye wimbo huo.
“Sawa unayo fedha, sasa hatua ya pili, kitu gani unaweza kukioffer
kwake, una kitu cha kuoffer kwa msanii wangu? Je wimbo ni mzuri? Kwahiyo
hivyo ndio vitu ambavyo unahitaji kuvifikiria. Na mwisho wa siku zote
unatakiwa kulinda brand yako.”
Kuhusu njia anayotakiwa msanii kufanikiwa katika soko la muziki wa
Marekani, Jason alisema jambo la kwanza ni kuwa na ukaribu na watu kama
yeye ambao wana connection na watu wengi pamoja na brands ambazo
zimesimama nchini humo. Geter alidai kufanya wimbo na msanii wa Marekani
peke yake, haitoshi kwa msanii wa Afrika kufanikiwa kwenye soko la
Marekani.
“T.I. alifanya ngoma na P-Square, lakini kiukweli, inahitaji zaidi ya
hivyo kupenya soko la Marekani,” alisisitiza Geter. “Inahitaji T.I. na
P-Square kwenda kwenye game ya basketball pamoja na kutembea pamoja.
Inahitaji uwekezaji huo wa muda kwa msanii wa Afrika kutumia muda kukaa
kwenye soko la Marekani.”
Geter alisisitiza kuwa kama msanii anataka kufanikiwa Marekani,
anatakiwa kutake risk kwa kuacha fedha nyingi anazopata Afrika na
kukubali kupata kidogo Marekani wakati anakuza jina lake. “Kama
unaingiza dola 5 Afrika, unaweza kuja Marekani na utakuwa na bahati sana
ukipata sehemu sahihi ambazo unaweza ukapata hata dola moja tu. Ni kazi
sana kwa watu kuwekeza muda wa aina hiyo na nguvu katika chochote kile,
hiyo ndio changamoto kubwa.”
Geter alisema hilo linawezekana kwa kuingia ubia na watu ambao tayari wana nguvu huko kukusaidia.
Kuhusu lugha ambayo msanii anatakiwa kutumia, Geter alisema muhimu ni
kufahamu kuongea Kiingereza lakini sio lazima nyimbo ziwe za lugha hiyo
kwakuwa muziki unaweza kufanya vizuri hata kama ukiwa umeimbwa kwa
lugha nyingine.
“Lakini yote ni kuwa kile ambacho tunafanana ni rhythm. Ni ile beat inayonifanya nicheze na pia hisia ambayo inagusa moyo. So
in America to get played on radio and all that stuff, yes you need to
know some English but if you got that beat right, we gonna move man.”
Msikilize zaidi hapa,.
Credit:- Bongo5
Post a Comment