Waje wa Nigeria asema wimbo aliomshirikisha Diamond utakuwa no 1 Afrika

Msanii wa kike Waje kutoka Nigeria ni miongoni mwa wasanii ambao watalishambulia jukwaa la Fiesta Jumamosi October 18 jijini Dar. Waje ambaye tayari amshaingia Dar alifanikiwa kumshirikisha staa wa Bongo Diamond Platnumz katika wimbo wake, kipindi Diamond alipoenda Naija miezi kadhaa iliyopita.
Waje ameusifia wimbo huo kwa kuupa nafasi ya kwanza barani Afrika pindi utakapotoka. “That song is so hot, that song should be number 1 in Africa by the time it comes out, so I’m not just going joking,” alisema kupitia XXL ya Clouds FM jana.
Ameongeza kuwa hajautoa wimbo huo hadi sasa sababu yupo chini ya uongozi ambao ndio huamua na kupanga kutoa nyimbo.
“Like I have a team a mananagement team, so it is not up to me alone but my team basically says okay this is the strategy we are going to use”.
Alimalizia kwa kusema kuwa hataki kurudia makosa ambayo amewahi kuyafanya kwa kutoa nyimbo bila kujipanga na mwisho wake hushindwa kufanya vizuri na kupotea.
“I have had experiences where you just throw out songs , they don’t pickup properly and then is just a waste.”

Post a Comment

Previous Post Next Post