Msanii wa kike Waje kutoka Nigeria ni miongoni mwa wasanii ambao
watalishambulia jukwaa la Fiesta Jumamosi October 18 jijini Dar. Waje
ambaye tayari amshaingia Dar alifanikiwa kumshirikisha staa wa Bongo
Diamond Platnumz katika wimbo wake, kipindi Diamond alipoenda Naija
miezi kadhaa iliyopita.
Waje ameusifia wimbo huo kwa kuupa nafasi ya kwanza barani Afrika pindi utakapotoka. “That song is so hot, that song should be number 1 in Africa by the time it comes out, so I’m not just going joking,” alisema kupitia XXL ya Clouds FM jana.
Ameongeza kuwa hajautoa wimbo huo hadi sasa sababu yupo chini ya uongozi ambao ndio huamua na kupanga kutoa nyimbo.
“Like I have a team a mananagement team, so it is not up to me
alone but my team basically says okay this is the strategy we are going
to use”.
Alimalizia kwa kusema kuwa hataki kurudia makosa ambayo amewahi
kuyafanya kwa kutoa nyimbo bila kujipanga na mwisho wake hushindwa
kufanya vizuri na kupotea.
“I have had experiences where you just throw out songs , they don’t pickup properly and then is just a waste.”
إرسال تعليق