RAY ATANGAZA MWISHO WA KOCHA PHIRI SIMBA NI KESHO TAIFA

Msanii wa filamu nchini, Vincent Kigosi ‘Ray’ ametamka kwa kujiamini kuwa Oktoba18, yaani kesho Jumamosi ndiyo siku ya mwisho kwa Kocha Mkuu wa Simba, Mzambia, Patrick Phiri raia wa Zambia kuifundisha timu hiyo.
Ray anadai kuwa sababu kubwa ni kuwa Simba itafungwa na Yanga kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika mechi baina ya timu hizo kwenye Ligi Kuu Bara.

“Kilichoipata Benin ilipokutana na Taifa Stars ndiyo kitaipata Simba itakapopambana na Yanga. Simba hauwezi kuifananisha hata kidogo na Yanga, wamekaa kambi Afrika Kusini ambako huko kwenyewe wanatoka sare tu,” alisema Ray ambaye ni shabiki mkubwa wa Yanga.
Msanii huyo amekuwa hakosi kwenye mechi za Ligi Kuu Bara hasa zile zinazoihusisha Yanga.
Hata hivyo, Phiri anaonekana ana asilimia 85 ya ushindi katika mechi zake zote alizokutana na Yanga. Amewahi kupoteza moja tu ingawa inaonekana kikosi chake kimeanza kwa sare tatu mfululizo, hali inayomlazimu kukiweka vizuri.

Post a Comment

Previous Post Next Post