Msanii wa
filamu nchini, Vincent Kigosi ‘Ray’ ametamka kwa kujiamini kuwa
Oktoba18, yaani kesho Jumamosi ndiyo siku ya mwisho kwa Kocha Mkuu wa
Simba, Mzambia, Patrick Phiri raia wa Zambia kuifundisha timu hiyo.
Ray
anadai kuwa sababu kubwa ni kuwa Simba itafungwa na Yanga kwenye Uwanja
wa Taifa jijini Dar es Salaam katika mechi baina ya timu hizo kwenye
Ligi Kuu Bara.
“Kilichoipata
Benin ilipokutana na Taifa Stars ndiyo kitaipata Simba itakapopambana
na Yanga. Simba hauwezi kuifananisha hata kidogo na Yanga, wamekaa kambi
Afrika Kusini ambako huko kwenyewe wanatoka sare tu,” alisema Ray
ambaye ni shabiki mkubwa wa Yanga.
Msanii huyo amekuwa hakosi kwenye mechi za Ligi Kuu Bara hasa zile zinazoihusisha Yanga.
Hata
hivyo, Phiri anaonekana ana asilimia 85 ya ushindi katika mechi zake
zote alizokutana na Yanga. Amewahi kupoteza moja tu ingawa inaonekana
kikosi chake kimeanza kwa sare tatu mfululizo, hali inayomlazimu
kukiweka vizuri.
إرسال تعليق