Matukio ya uhalifu wa ubakaji na ulawiti yameongezeka mkoani Iringa ikilinganishwa na mwaka jana.
Kamanda wa polisi mkoani Iringa ACP. Ramadhani Mungi amesema jeshi lake limepokea matukio ya ubakaji na ulawiti 21 kwa kipindi cha mwezo Januari hadi Septemba mwaka huu.
Kamanda Mungi amesema jeshi lake linaendelea na msako dhidi ya watu ambao huwarubuni watoto na kuwanyia vitendo vya ulawiti na ubakaji.
Aidha, amewashauri wazazi na walezi kufuatilia mienendo ya watoto wao pindi wanapocheza ili kupunguza vitendo vya ubakaji na ulawiti katika jamii.Hata hivyo, kamanda wa polisi mkoani Iringa amewakumbusha wananchi kutoa taarifa za uhalifu kwa jeshi lake ili kupambana na vitendo hivyo.

إرسال تعليق