Jon Schultz
Mfanyabiashara mmoja
ameamua kutumia ‘fursa’ aliyoiona kupitia janga la Ebola linalosumbua
maeneo mbalimbali ya dunia kwa sasa, kwa kuuza domain ya www.ebola.com
kwa pesa nyingi.
Jon Schultz anaiuza domain hiyo kwa $ 150,000 sawa na zaidi ya shilingi milioni 250.
Jamaa huyo anayejiita
‘domain entrepreneur’ aliinunua domain hiyo miaka minne iliyopita
(2008) kwa $13,500 sawa na zaidi ya shilingi milioni 22, na amedai kuwa
alikuwa akisubiri wakati muafaka wa kuiuza.
“Ebola.com would
be a great domain for a pharmaceutical company working on a vaccine or
cure, a company selling pandemic or disaster-preparedness supplies, or a
medical company wishing to provide information and advertise services” Schultz aliiambia CNBC.
Kwa mujibu wa Daily
Mail, Schultz piz anamiliki domain zingine kama H1N1.com, birdflu.com,
terror.com, PotassiumIodide.com, fukushima.com.
إرسال تعليق