Na Abdulaziz Ahmed, Lindi
Watu
wawili wamekufa na wawili kujeruhiwa baada ya gari waliyokuwa
wanasafiria kuacha njia na kupinduka katika kijiji cha Michenga, wilaya
ya Ruangwa Ruangwa mkoani Lindi.
Kamanda
Mzinga aliwataja waliokufa kwenye ajali hiyo kuwa ni Binasa Mapua(51)
mkazi wa Tabata Dar-eS-salaam na Elizabeth Chipoleka(53),mkazi wa Yombo,
Dar es salaam.
Kamanda
Mzinga amewataja waliojeruhiwa kuwa ni Mussa Mchalanganya na Rashid
Mchalanganya ambaye ni mwanafunzi katika Chuo cha Usafirishaji (NIT),
ambapo wote ni wakaazi wa Tabata, Dar es salaam. Dereva wa gari hilo
ametiwa mbaroni na upelelezi unaendelea kujua chanzo hasa cha ajali hio.
إرسال تعليق