|
Mbunge
wa Jimbo la Kisesa (CCM), Luhaga Mpina akizungumza na wananchi wa
Kijiji cha Mwandu Itinje wilayani Meatu mkoani Simiyu, waliofika eneo
hilo kushuhudia mpambano ulioandaliwa na mbunge huyo wa ngoma za asili
ya watu wa kabila la Wasukuma kati ya Malogi Hamsini na Magise Jilunga. |
MBUNGE
wa Jimbo la Kisesa(CCM), Luhaga Mpina ameahidi kuendelea kuenzi
utamaduni wa ngoma za kabila la wasukuma kwani zimekuwa ni sehemu ya
kuimarisha mshikamano miongoni mwa jamii hiyo.
Mpina
alitoa kauli hiyo juzi wakati akifunga mpambano wa ngoma za asili
katika Kijiji cha Mwandu Itinje wilayani Meatu mkoani Simiyu
uliwakutanisha Malogi Hamsini Mgika na Magise Jilunga Mgalu.
Hata
hivyo katika mpambano huo ulihudhuriwa na watazamaji zaidi elfu nane
kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Simiyu ambapo Magise Jilunga
aliibuka mshindi baada ya kumbwaga Malogi.
Akizungumza
mara baada ya mpambano huo, Malogi Hamsini alikubali kushindwa na
mpinzani wake na kueleza kuridhika na uamuzi uliofanywa na kuomba
kukutanishwa tena siku nyingine na mpinzani wake huyo.
Naye
Magisa Jilunga alisema pamoja na kumshinda mpinzani wake lakini alikiri
pambano hilo lilikuwa gumu kwake na kuamba nae pia kurudiana ombi
ambalo lilikubaliwa na Mbunge wa jimbo hilo.
Pambano
hilo lililodhaminiwa na Mbunge Mpina lilivuta hisia za mashabiki wengi
na kuomba kufanyika mara kwa mara kwa pambano hilo kwani linaleta umoja
na mshikamano miongoni mwa jamii.
Mpina
aliwazawadia shilingi milioni moja kila mmoja katika mpambano huo na
kuahidi kudhamini tena pambano lingine kama hilo baadae mwakani. ZAIDI BOFYA PLAY KUSIKILIZA YALIYOJIRI.
|
Wachezaji wa ngoma toka kundi la Malogi Hamsini ambaye ni Mgika wakifanya yao. |
|
Mbunge wa Jimbo la Kisesa (CCM), Luhaga Mpina akipiga ngoma kuashiria ufunguzi wa mpambano wa ngoma asili kati ya Malogi Hamsini na Magise Jilunga. |
|
Kiongozi
wa Wagika, Malogi Hamsini (kulia) akiwa amesimama barabara kuuanza
mpambano ambapo alizidiwa nguvu ya uchawi na Mpinzani wake Magise
Jilunga ambaye Mgalu. |
|
Wachezaji wa kundi la Malogi Hamsini wakionyesha kazi. |
|
Mara
baada ya kuona ameshindwa katika nguvu za kichawi Malogi Hamsini
alipandwa na hasira ampazo alizielekeza kweye tunguli zake. |
|
Na hapo ndipo alipo amua kuziteketeza kwa kuzifumua kwa mateke..... PwachAaA!! |
|
Wingi
wa watu ndiyo pointi za ushindi watu walihama toka kwa Malogi Hamsini
na kuelekea kwa Magise Jilunga ambapo kila mmoja alikuwa akipiga ngoma
kwa wakati mmoja (yaani kulia na kushoto wapi pananoga?). |
|
Wananchi wakiwa wameizunguka himaya ya Magise Jilunga. |
|
Kiongozi
wa Wagalu, Magise Jilunga wa pili kutoka kushoto akiwa tayari
kulianzisha kwenye mpambano kati yake na Malogi Hamsini ulioandaliwa na
Mbunge wa Jimbo la Kisesa Luhaga Mpina. |
|
Hatari kama anaporomoka vile... |
|
Malogi Hamsini alituma nyoka kuja kuharibu ngoma ya Magise Jilunga lakini hakufua dafu. |
|
Mapanga dizaini.... |
|
Akinamama wakiingia kwenye lango kuu kushuhudia mpambano. |
|
Michezo ya hatari balaa ni mwendo kugalagala kwenye moto. |
|
Silaha ya ushindi kwa Magise Jilunga ilikuwa ni kubadilika badilika. |
|
Si kubadilika tu bali alikuwa na vionjo kama kuoga moto mchana kweupe na kunywa mafuta ya dizeli...tobA! |
|
Ni balaa mwanawane!!! |
|
Jamaa aliamua kukizika kichwa kwa dakika kadhaa kiasi cha kusisimua mashabiki!! |
|
Kiongozi wa Wagalu, Magise Jilunga akipiga ngoma kuusaka ushindi. |
|
Viongozi wa kada mbalimbali nao wamo. |
|
Mbunge
wa Jimbo la Kisesa (CCM), Luhaga Mpina akizungumza na wananchi wa
Kijiji cha Mwandu Itinje wilayani Meatu mkoani Simiyu, waliofika eneo
hilo kushuhudia mpambano ulioandaliwa na mbunge huyo wa ngoma za asili
ya watu wa kabila la Wasukuma kati ya Malogi Hamsini na Magise Jilunga. |
|
Maelfu
waliofika eneo hilo kushuhudia mpambano ulioandaliwa na Mhe. Mbunge,
ngoma za asili ya watu wa kabila la Wasukuma kati ya Malogi Hamsini na
Magise Jilunga. |
|
Ni
wakati wa jaji Mkuu kutangaza matokeo rasmi:- Mpambano wa ngoma za
asili ya watu wa kabila la Wasukuma kati ya Malogi Hamsini na Magise
Jilunga. |
|
"Mshindi ni Magise Jilunga...!!" |
|
Malogi Hamsini (kushoto) akimpongeza kiroho safi Magise Jilunga mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi.... |
|
Full m-banano. |
|
Mbunge wa Jimbo la Kisesa (CCM), Luhaga Mpina akiwaaga wananchi wa Jimbo lake mara baada ya kumalizika mpambano. |
|
Mbunge wa Jimbo la Kisesa (CCM), Luhaga Mpina akiwaamezungukwa na maelfu ya wananchi waliofika eneo la uwanja wa kusanyiko. |
إرسال تعليق