Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bi. Doroth Mwanyika (kushoto) akitia saini
mkataba wa ushirikiano wa Mpango wa Mageuzi ya Usimamizi wa Fedha za
Umma (PFM) Awamu ya IV kwa niaba ya Serikali ya Tanzania leo jijini Dar
es salaam. Kulia ni Balozi wa Finland nchini Bi. Sanikka Antila.
Na Eleuteri Mangi –MAELEZO
Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepokea Sh. Bilioni 10.1 ambazo ni
sawa na EURO milioni 4.8 kutika Serilkali ya Finland ikiwa kwa lengo la
ushirikiano wa Mpango wa Mageuzi ya Usimamizi wa Fedha za Umma (PFM)
Awamu ya IV.
Mkataba
wa makubaliano hayo umesainiwa leo jijini Dar es salaam na Naibu Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha Bi. Doroth Mwanyika kwa niaba ya Serikali ya
Tanzania na Balozi wa Finland nchini Bi. Sanikka Antila.
Bi.
Doroth amesema kuwa Mpango wa Mageuzi ya Usimamizi wa Fedha za Umma
Awamu ya nne ametanguliwa na Awamu ya I hadi III ambapo awamu hizo
zimeonesha mafanikio mbalimbali nchini.
Mafanikio
hayo ni pamoja na ongezeko la ukusanyaji wa mapato kutoka Sh. Bilioni
390 mwaka 2009/2010 hadi zaidi ya Sh. Bilioni 700 kwa mwezi mwaka
2013/2014 na kuboresha mifumo ya kifedha kwa kutumia mifumo ya
kielektroniki kwa kulipa moja kwa moja kwenye akaunti husika.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bi. Doroth Mwanyika (kushoto)
akibadilishana hati ya mkataba wa ushirikiano wa Mpango wa Mageuzi ya
Usimamizi wa Fedha za Umma (PFM) Awamu ya IV waliosaini leo jijini Dar
es salaam. Kulia ni Balozi wa Finland nchini Bi. Sanikka Antila.
Bi
Doroth metaja mafanikio mengine kuwa ni ubureshwaji wa utendaji
watumishi wanaosimamia masuala ya mpango wa PFM kupitia Ofisi ya Mkaguzi
Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) na utendaji kazi mzuri wa
kamati za Bunge zinazohusika na ufuatiliaji wa matumizi ya Fedha za
umma.
Aidha,
Bi. Doroth ameishukuru Serikali ya Finland kwa ushirikiano mzuri
wanaoendelea kuipa Tanzania na kuahidi kuwa fedha hizo zitatumika katika
malengo yaliyokusudiwa katika kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo
kupunguza umasikini nchini.
Naye
Balozi wa Finland nchini Bi. Sanikka Antila amesema kuwa usimamizi
mzuri wa fedha za umma (PFM) umeifanya nchi yake kuongeza fedha kwa
ajili ya mpango huo.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bi. Doroth Mwanyika (kushoto) akishukuru
Serikali ya Finland kwa ushirikiano mzuri wanaoendelea kuipa Tanzania
mpaka sasa na kuahidi kuwa fedha hizo zitatumika katika malengo
yaliyokusudiwa. Kulia ni Balozi wa Finland nchini Bi. Sanikka Antila.
“PFM
ni muhimu kwa utawala wa kidemokrasia, uchumi imara, ufanisi katika
matumizi ya rasilimali zilizopo na hivyo kupunguza umasikini” alisema
Bi. Sanikka.
Ufanisi
wa usimamizi mzuri wa fedha za umma umewezesha ufanisi wa malighafi
zilizopo nchini katika kuboresha elimu, kutoa huduma bora za kiafya,
kuongeza mazao ya kilimo na kuendeleza utalii.
Mpango
wa PFM upo katika awamu ya nne na ulianza 2012 na unatarajiwa kuishia
2017 ambapo awamu ya I hadi III ilianza 1998 na kumalizika 2012, Finland
imekuwa nchi ya sita mhisani katika kusaidia mpango huu wa mageuzi.
Nchi nyingine wahisani ni pamoja na Canada, Ujerumani Ireland na Uingereza.
Balozi
wa Finland nchini Bi. Sanikka Antila (kulia)PFM akiongea na waandishi
wa habari (hawapo pichani) na kuipongeza kwa kusimamia fedha za umma na
kuwa na uongozi unaosimamia utawala wa kidemokrasia, uchumi imara,
ufanisi katika matumizi ya rasilimali zilizopo na hivyo kupunguza
umasikini. Hafla hiyo imefanyika leo jijini Dae es salaam wakati wa
kusaini mkataba wa ushirikiano wa Mpango wa Mageuzi ya Usimamizi wa
Fedha za Umma (PFM) Awamu ya IV. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya
Fedha Bi. Doroth Mwanyika.
Baadhi
ya waandishi wa habari waliohudhuria hafla ya kusaini mkataba wa
ushirikiano wa Mpango wa Mageuzi ya Usimamizi wa Fedha za Umma (PFM)
Awamu ya IV kati ya Serikali ya Tanzania na Finland leo jijini Dar es
salaam.(Picha zote na Eleuteri Mangi- MAELEZO)
إرسال تعليق