Meneja
wa Mkoa wa Tabora Bw. Erasto Chilambo, akimpa maelezo ya ujenzi wa
nyumba za gharama nafuu Mkuu wa Mawasiliano na Huduma kwa Jamii Bi Susan
Omari alipotembelea mradi huo ulioko eneo la Isikizya Wilayani Uyui
jana. (Picha kwa hisani ya Kitengo cha Mawasiliano ya Umma na Huduma kwa
Jamii cha Shirika la Nyumba la Taifa).
Mwonekanao wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC eneo la Isikizya Mkoani Tabora.
Meneja
wa Mkoa wa Tabora Bw. Erasto Chilambo akiendelea kutoa maelezo ya mradi
kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii, Bi Susan
Omari.
Nyumba
38 zilizojengwa karibu kabisa na Makao Makuu ya Wilaya ya Uyui eneo la
Isikizya. Nyumba zingine 12 zimejengwa upande wa pili wa barabara eneo
la Isikizya.
Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Jamii wa NHC, Bi Susan Omari akitoa maelekezo kwa Meneja wa Mkoa wa Tabora Bw. Chilambo.
Msimamizi
wa mradi wa NHC isikizya Bw. Tokimu Mondo akitoa maelezo ya utekelezaji
wa mradi wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu eneo la Isikizya jana.
Sehemu ya nyumba zilizojengwa katika mradi wa nyumba za gharama nafuu eneo la Isikizya Wilayani Uyui zinavyoonekana.
Meneja
wa Mkoa wa Tabora Bw. Chilambo akitoa maelezo kwa Mkuu wa Kitengo cha
Mawasiliano na Huduma kwa Jamii Bi. Susan Omari yanayohusu viwanja vya
Shirika vilivyoko eneo la Itetemia Manispaa ya Tabora.
Meneja
wa Mkoa wa Tabora Bw. Erasto Chilambo akielezea hatua mbalimbali
zilifikiwa na Mkoa huo za kutengeneza nyumba za Shirika. Hili ni
mojawapo ya jengo la Hoteli ya Golden Eagle baada ya kufanyiwa
matengenezo.
Sehemu ya mtaa wa Jamhuri/Shule wenye nyumba zilizofanyiwa matengenezo makubwa na NHC Mkoa wa Tabora.
Mojawapo wa jengo lililofanyiwa matengenezo na NHC Mkoa wa Tabora linavyoonekana kwa sasa.
Sehemu
ya Maafisa Vijana wakisikiliza mada iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha
Mawasiliano na Huduma kwa Jamii wa NHC, Bi Susan Omari (hayuko pichani)
alipoelezea mpango wa NHC wa kugawa mashine kwa ajili ya kusaidia vijana
kwenye Halmashauri zote za Wilaya hapa nchini. Jumla ya mashine 656
zimeshambazwa kwa ajili hiyo.
Washiriki wa semina iliyotolewa na NHC wakisikiliza mada kwa makini.
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii wa NHC, Bi Susan Omari
akitoa mada juu ya mpango wa NHC wa kusaidia vijana mashine za
kufyatulia matofali katika Halmashauri zote za Wilayanchini.
Mmoja
wa washiriki wa semina hiyo akilishukuru Shirika la Nyumba la Taifa kwa
uamuzi wake wa kizalendo wa kusaidia vijana mashine ili waweze
kujiajiri alipochangia mada iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha
Mawasiliano na Huduma kwa Jamii wa NHC.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, , Bibi Sihaba
Nkinga akitoa maelezo wakati wa semina iliyotolewa na NHC mjini Tabora
jana.
إرسال تعليق