Mahmoud Ahmad Arusha
SERIKALI imesema kuwa inachukua
hatua mbalimbali ambazo kudhibiti mauaji ya Tembo wanazidi kuteketea na
kuangamia dunia kama ambayo yanafanywa na wachache ambao wanatamaa ya
kujipatia utajiri.
Hayo yameelezwa na waziri wa
Maliasili na Utalii, Lazaro Nyarandu, kwenye kilele cha matembezi ya
kupinga mauaji ya Tembo na Faru yaliyoandaliwa na Chama cha waongoza
watalii, TATO, yaliyofanyika jijini Arusha kwenye uwanja wa mpira wa
Sheikh Amri Abeid.
Amesema mwaka 1940 duniani
kulikuwa na Tembo milioni 10 , lakini kutokana na kuongezeka kwa mauaji
tembo inakadiriwa kuwa mwaka 2014 dunia kutakuwa na tembo 4002 tu na
hiyo inashiria kuwa tembo wanauliwa kwa kasi kubwa mno.
Waziri Nyalandu,amesema miaka
miwili iliyopita ameshaiagiza Taasisi ya utafiti wa wanyama pori nchini
TAWIRI na shirika la wanyama pori la Ujeruman, la Frank fut Zological na
wadau wengine wa utalii kufanya sensa ya tembo katika mbuga zote
nchini .
Amesema rais Kikwete, alipokuwa
mjini London, Uingereza, alikutana na mtoto wa Malkia. Prince Charles,
na kueleza kuwa Tanzania imeshapiga marufuku biashara ya meno ya tembo
na ghala la meno ya tembo ambalo lina akiba ya tani 130,000,zitalindwa
na Tanzania kwa kushirikiana na Uingereza, Umoja wa mataifa ili
kudhibiti wizi wa pembe hizo.
Nyalandu, amesema katika
kukabiliana na ujangili huo tayari serikali imeshawakamata majangili
15,412, na silaha aina mbalimbali zilizotumika kwenye mauaji ya tembo
ambazo ni AK 47 ,na Automatiki rifle ambazo zitateketezwa hivi karibuni
kwa kuwa zikiachwa zinaweza kuingia kwenye mikono isiyo salama na
kusababisha ujambazi
Waziri Nyalandu, ametumia fursa
hiyo kuziomba nchi za China, Japan, Thailand ,Korea ya kusini ,na
kaskazini ,Vietnam, kuacha kununua meno ya tembo na pembe za faru ili
kuokoa mauaji ya wanyama hao
.Awali mwenyekiti wa Chama cha
waongoza Utalii, TATO, Wilium Chamburo, ameiomba serikali kuangalia
uwezekano wa kuwamilikisha wanavijiji waishio kandokando ya hifadhi
kumilikishwa maliasili zilizopo ili waweze kusaidia ulinzi na udhibiti
wa mauaji ya tembo.
إرسال تعليق