Unataka kwenda kwenye ajira ambayo huijui au huna uzoefu nayo.
Mara nyingi kutokuwa na uzoefu ni kitu ambacho kinawasumbua wengi na
wakati mwingine unajihisi huwezi kupata fursa au kazi fulani.
Kama unataka kupata ajira mpya kwenye kampuni fulani, unatakiwa kujua
utaleta kitu gani kwenye nafasi hiyo unayopewa. Si mara zote wanahitaji
mtu mwenye uzoefu ila mtu amabaye yuko tayari kufanya kwa viwango vyao
hata kama hana uzoefu ndio maana wanatoa miezi mitatu ya majaribio.
Hebu angalia sababu hizi zinaweza kukusaidia kupata kazi hata kama huna uzoefu;
- Unahitaji kuona Mambo kitofauti kutokea ngazi ya chini
Wote tunaanzia chini wakati fulani, hivyo kile unachokifanya sasa si
lazima kuwa ndio hicho utakachokifanya maisha yako yote. Hivyo unatakiwa
kubadilisha mfumo wako wa kufikiri unapoanza kutafuta kazi. Fanya kitu
ambacho ni kidogo ambacho kitakuongezea uzoefu ule unaohitajika kwa kazi
fulani. Hakuna kitu kidogo au ukasema huna uzoefu ila ni jinsi gani
unafanya mambo yako kwaajili ya kukupa uzoefu.Unapoanza bila kitu katika
kitu ambacho unakitaka katika taaluma au biashara ingawa wengi
tunaogopa mabadiliko na kushindwa. Usiogope fursa kabla haujaijaribu,
unahitaji kuanza mahali fulani ili uweze kuelekea sehemu nyingine. Ni
kweli huna uzoefu je unafanya nini ili kukusaidia kupata uzoefu wa ile
kazi unayoiota?
- Unatakiwa kuwa mbunifu katika fikra zako hicho ndicho kitu cha muhimu
Uwezo wako wa kuboresha ni kitu muhimu unapoboresha na kuendeleza
taaluma yako. Haijalishi unataka kubadilisha taaluma au kupanda cheo
unatakiwa kuwa mbunifu wa kila unachofanya ili uwe tofauti na mtu
mwingine katika kitengo chako. Kwa lugha nyingine wewe unatofautishwaje
na mtu mwingine mwenye cheti kama cha kwako?
Wahitimu wengi wa sasa hawajui teknolojia vizuri na wanaichukulia na
kama kitu ambacho si cha muhimu sana mpaka uwe masomo ya sayansi. Kama
unataka kuongeza ubunifu wako katika mawazo yako hakikisha unakwenda
sambamba na teknolojia utajikuta fikra na mawazo yako yanakuwa tofauti
na watu wengine katika eneo hilo hilo.
Ogopa kuwa mtu ambaye hujui nini kinaendelea kwenye teknolojia
inayohusiana na kazi yako au taaluma yako unayoitaka. Unahitaji kujua
program za komputa zinazohusiana na kazi yako vizuri, usisubiri kwamba
utaenda kufundoshwa ukiajiriwa au kupata kazi ndipo unaanza kuhangaika
kujifunza. Jifunze leo kiweze kukusaidia kesho.
- Kwasababu Wengine Wameweza na imewezekana
Mawazo yetu finyu wakati mwingine hufikiri mambo hayawezekani
kwasababu hatujaona walioweza kufanikiwa au kufanya. Haimaanishi wewe
kutojua kitu fulani basi watu wengine duniani hawajui kuhusu hicho bali
unatakiwa ujue kama wewe hujui kuna mtu anajua na anaweza kukusaidia
kutoka hapo ulipo kwenda hatua nyingine. Hutakiwi kukaa ukafikiri ni
mwisho wa dunia hutotoka hapo, jaribu kufanya kitu na itawezekana hata
kwa kujitolea fanya tu itakusaidia kukupa ujuzi. Kuna wengine wamepata
kazi kwa sababu walijitolea kufanya kwa malipo ya kujikimu au kutolipwa
kabisa na wakapata uzoefu ambao ukawasaidia kufikia ile kazi
walioitamani. Kama huna uzoefu unafanya jitihada gani kutafuta huo
uzoefu na kazi unaohitaji?
Jifunze vitu mbali mabali ingawa huna uzoefu vitakusaidia kufikia
malengo na hatua fulani unayoitamani. Usikae tu kama pakacha bovu, fanya
kitu ushindani ni mkubwa sana.
إرسال تعليق