Katika
hali isiyo ya kawaida mechi kati ya Serbia na Albania imeshindwa
kumalizika baada ya ndege isiyokuwa na rubani kubeba ujumbe wa kisiasa
kusababisha vurugu zilizowahusisha wachezaji na mashabiki ndani ya
uwanja wa Partizan.
Mechi hiyo ya kufuzu katika michuano ya soka
bara la Ulaya mwaka 2016 ilisimamishwa na mwamuzi Martin Atkinson kutoka
Uingereza katika dakika ya 41 ya mchezo huo huku matokeo yakisomeka
0-0.
Vurugu ziliibuka wakati bendera ya Albania na ujumbe
kupeperushwa juu ya uwanja na kushikwa na wachezaji wa Serbia. Wachezaji
wa Serbia walijaribu kuichukua bendera hiyo mbele ya mashabiki kadhaa
ilichanika ndani ya uwanja.
'Tukio moja la kijinga limesababisha
vurugu- hiyo ndio njia ya mkato kulielezea tukio lililotokea usiku'
alisema mwandishi wa televisheni ya B92 Milos Saranovic.
Mwamuzi
Atkinson aliwaondoa wachezaji nje ya uwanja na baada ya kuchelewa kwa
dakika 30 Uefa ilithibitisha kusitishwa kwa mchezo huo.
Serbia na
Albania wanahistoria ya kutoelewana mara kwa mara ikihusishwa na jimbo
la zamani la Serbia Kosovo jimbo ambalo lilijipatia uhuru mwaka 2008.
إرسال تعليق