Viongozi
wa kimila wa kabila la wamasai waishio katika vijiji vitano
vinavyozunguka uwanja wa ndege wa kimatifa (KIA)wamepinga agizo la
waziri wa nyumba, ardhi na makazi Prof. Anna Tibaijuka la kuwataka
waondoke katika maeneo yao kwa ajili ya kupisha upanuzi wa uwanja bila
kuwasikiliza.Wakizungumza kwenye kikao cha kujadili mgogoro huo viongozi
hao wamemtaka waziri Tibaijuka kufika katika vijiji hivyo na
kuwasikiliza wananchi badala ya kutoa maagizo ya kuhamishwa akiwa
ofisini kwa kuwa mgogoro huo tayari wameufikisha katika ofisi ya waziri
mkuu na kwamba wanasubiri majibu ya tume iliyoundwa.Wamesema hawako
tayari kuondoka katika maeneo hayo ambayo uwanja uliwakuta na kwamba
tayari wameshajiimarisha na kuweka miundombinu ya zahanati shule, afya,
maeneo ya kilimo na malisho ya mifugo.
Kwa
upande wake diwani wa kata ya KIA Mh.Sinyork Ole Nanyoki amesema
wananchi wa vijiji hivyo wana hati miliki ya maeneo yao licha ya
serikali kutoa hati miliki bandia kwa uongozi wa kiwanja cha ndege, na
kwamba ni vema viongozi wa serikali wakatumia busara kutatua mgogoro huo
ambao unaweza kuhatarisha amani.
Akizungumza
na watendaji wa idara ya ardhi katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa
Kilimanjaro waziri wa nyumba ardhi na makazi Prof Anna Tibaijuka alisema
haoni sababu ya wananchi kuendela kuishi katika maeno hayo badala yake
wapewe fidia ili kupisha uwanja wa ndege.
إرسال تعليق