‘Bunge kukwamisha bajeti Wizara ya Ujenzi’


Kyela. Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imesema kuwa haitapitisha bajeti ya Wizara ya Ujenzi kwa kile kilichoelezwa kubaini uozo wa ujenzi usiokidhi kiwango katika miradi ya miundombinu ya barabara wilayani Kyela mkoani Mbeya, ikieleza kwamba italazimika kutembea nchi nzima ili kujiridhisha na miradi hiyo.
Kauli hiyo imetolewa juzi katika majumuisho ya ziara ya kamati hiyo iliyoongozwa na Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe iliyotembelea Bandari za Itungi na Kiwila kujua shughuli mbalimbali za kiuchumi zinazoendelea.
Wakiwa njiani, msafara huo ulisimamishwa mara tatu na wananchi na wengi wakieleza kero yao kuwa ni ubovu wa miundombinu.
Akizungumza katika ziara hiyo, mbunge Viti Maalumu, Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar, Maryam Msabaha alisema kuwa kitendo kilichotokea wilayani Kyela ni cha aibu na kwamba kamati hiyo haitavumilia uozo huo unaofanywa na wizara na halmashauri kushindwa kusimamia kikamilifu makandarasi wanaopewa zabuni na kusababisha Serikali kushushiwa mzigo wa lawama.
“Magufuli ni jamaa yangu, sitasita kumweleza ukweli na kwamba bajeti yake haiwezi kupitishwa bila kamati hii kuzunguka nchi nzima ili kujiridhisha na miradi ya ujenzi wa miundombinu. Anapaswa kutambua fedha zinazotumika katika miradi hiyo ni kodi za wananchi na ni haki yao kulalamika,” alisema

Post a Comment

أحدث أقدم