Dar es Salaam. Klabu za Simba na Yanga
zimefanya mabadiliko kwenye vikosi vyao na moja kwa moja watakuwa
wameathiri nafasi za baadhi ya wachezaji wa vikosi hivyo.
Timu zote hizo kongwe zimefanya mabadiliko zaidi
katika kujiimarisha lakini pamoja na mapendekezo mapya yaliyowekwa,
imewaweka pabaya baadhi ya wachezaji na hivyo kufanya wakati wao kuwa
mgumu.
Yanga imewasajili Mliberia Kpah Sherman, Mrundi
Amissi Tambwe na Danny Mrwanda kwenye safu ya ushambuliaji na kipa
Athumani Majogo, wakati Simba imewasajili Dan na Simon Sserunkuma, Juku
Musheed (wote raia wa Uganda) na Hassan Kessy. Wafuatao watakalia kuti
kavu Simba kipindi hiki;
William Lucian ‘Gallas’
Usajili wa Hassan Kessy aliyetokea Mtibwa Sugar
utampa wakati mgumu beki huyu na kwamba anaweza kuwa chaguo la pili kama
si la tatu. Licha ya kuwa na uzoefu na umri wake bado ukiwa mdogo,
Lucian atakuwa na wakati mgumu wa kupata nafasi mbele ya Kessy, ambaye
amekuwa akiwindwa na Simba kwa kipindi kirefu bila mafanikio hapo awali.
Nassor Masoud ‘Chollo’
Beki huyu mkongwe wa Simba ameonekana kurudisha
makali yake hivi karibuni, lakini inasadikiwa uwepo Kessy utamrudisha
tena benchi.
Chollo hajawa na kipindi kizuri kwa takribani
mwaka sasa kutokana na matatizo ya majeraha. Chollo uenda akawa mbadala
wa Kessy kwenye kikosi cha kwanza cha Simba.
Hassan Isihaka:
Hakika amekuwa akifanya kazi kubwa na hata
kuaminika kuanza kwenye michezo yote ya kirafiki na ya ligi kwa msimu
huu. Isihaka amekuwa akicheza sambamba na Joseph Owino lakini hali
ilivyo sasa baada ya usajili wa beki Juku Musheed, huenda akapoteza
nafasi.
Shaban Kisiga ‘Marlone’
Licha ya kuwa na uwezo mkubwa wa kuichezesha timu
na kufunga mipira ya faulo. Kiungo huyo mshambuliaji anaweza kupoteza
nafasi kwa washambuliaji Dani Sserunkuma na Elius Maguli ambao ni chaguo
la kwanza la Kocha wa Simba Patrick Phiri aliyetokea kwenye klabu ya
Gor Mahia ya Kenya.
- Mwananchi
- Mwananchi
إرسال تعليق