Askari
mmoja wa Jeshi la Polisi amefariki dunia na wengine watano
wamenusurika kufa baada ya boti waliyokuwa wamepanda kwa ajili ya
kufanya doria kupinduka katika Bahari ya Hindi.
Ajali hiyo ilitokea juzi saa saba usiku eneo la Jambiani, Mkoa wa Kusini Unguja wakati askari hao wakiwa katika doria.
Akizungumza na NIPASHE, Kamanda wa Polisi mkoa wa Kusini Unguja, Juma Sadi Khamis, alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa boti hiyo ilikuwa na askari sita, mmoja wa Kikosi Maalum cha Kuzuwia Magendo Zanzibar (KMKM).
Kamanda Juma alisema wanane waliokolewa na ni majeruhi na kwamba mmoja hajapatikana.
Alimtaja aliefariki dunia ni askari wa Jeshi la Polisi F7642 Saidi Hassan Saleh (36) na majeruhi ni G1320 PC Mahmoud, F4578 PC Haji Khamis, E837 koplo Mbaraka na K1627 PO Faridi Muhammed Suleiman wa KMKM.
“Hadi sasa bado mtu mmoja hajapatikana ambaye ni ASP Tenga, ni askari polisi na juhudi za kumtafuta zinaendelea na mwili wa askari aliefariki tumeshampeleka hospitali ili kuweza kuukabidhiwa jamaa zake kwa ajili ya mazishi,” alisema Kamanda Juma.
Alisema chanzo cha ajali hiyo ni mashine za boti hiyo na kuanza kujaa maji kishakupinduka. Aliyataja mawimbi kuwa nayo yalichangia kusababisha ajali hiyo.
Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdani Omar, alisema majeruhi hao hali zao ni nzuri na kwamba polisi walikuwa katika eneo la tukio wakisaidiana na wananchi wa kijiji hicho kutafuta askari ambaye hajaonekana.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri Zanzibar (ZMA), Abdi Maalim, alisema ni mara ya kwanza kwa boti za doria za polisi kupata ajali huku akiwataka manahodha na wenye vyombo vya baharini kuchukua tahadhari hasa katika kipindi hiki cha upepo mkali baharini.

CHANZO:
NIPASHE
إرسال تعليق