Tusiime yatoa wanafunzi 18 bora Dar

Ofisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mapunda.
Shule ya Msingi Tusiime ya jijini Dar es Saam, imeendelea kufanya vizuri ambapo safari hii wanafunzi 18 bora kwa Mkoa wa Dar es Salaam wametoka katika shule hiyo.
Hayo yamo kwenye taarifa ya Ofisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mapunda, kuhusu uchaguzi wa wanafunzi kujiunga kidato cha kwanza katika shule za serikali mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, waliofanikiwa kuingia 10 bora kwa upande wa wavulana wanafunzi wanane wanatoka Tusiime na wengine wawili wanatoka shule za Mounteverest na Fountain wakati 10 bora kwa wasichana wote wametoka Tusiime.

Taarifa hiyo inaonyesha pia wanafunzi wa Tusiime wamechaguliwa kujiunga na shule za vipaji maalum  sehemu mbalimbali nchini.

Ilisema wavulana na wasichana 10 bora wote wametoka Manispaa ya Ilala na Kinondoni na kwamba shule nyingi zilijiandaa vyema katika uendeshaji wa mtihani wa kumaliza elimu ya msingi.

Hata hivyo, taarifa iliongeza kuwa changamoto inayokabili baadhi ya shule za serikali miaka ijayo ni uhaba wa vyumba vya madarasa vinavyohitajika katika mitihani kutokana na wingi wa watahiniwa.
CHANZO: NIPASHE

Post a Comment

أحدث أقدم