Albert Pike alitabiri vita kuu tatu za dunia-2

Inaendelea kutoka wiki iliyopita. Albert Pike alifanya kazi zake kwa ukaribu na Giusseppe Mazzini wa Italia (1805-1872) ambaye alikuwa ni mwashi huru mwenye digrii 33, ambaye alikuwa ni mkuu wa Illuminati mnamo mwaka 1834, na ndiye mwanzilishi wa kundi la Mafia mnamo mwaka 1860.

Wengine aliofanya nao kazi kwa ukaribu ni Adriano Lemmi (1822-1896) na baadhi ya viongozi mashuhuri wa ulimwengu kama vile Lenin, Trosky na baadaye Stalin, lengo likiwa ni kuziangusha tawala mbalimbali za kifalme za Ulaya na kuanzisha tawala za kimapinduzi yakiwa ni maandalizi ya kuanzisha utawala mmoja tu ulimwenguni. Huu ulikuwa ni mwendelezo wa falsafa ya illuminati ambayo ilianzishwa na Adam Weishaupt.

Kati ya mwaka 1859 hadi 1871 aliandaa mpango mkakati wa kuanzisha vita kuu tatu za dunia na mapinduzi matatu makubwa akitabiri kuwa matukio yote hayo yangetokea katika karne ya 20.

Ili yaliyotabiriwa yatokee kama ilivyopangwa, Pike aliamini kuwa falsafa za Ukomunisti, Ufashisti na Uzayuni, ambazo ni matokeo ya kazi za waashi huru, zingetumika kuchochea vita na mapinduzi duniani.

Ikumbukwe kuwa mnamo mwaka 1829 katika mkutano wao wa New York, waashi huru walitangaza kuwaunganisha watu wote wasioamini uwepo wa Mungu katika mwavuli mmoja wa Ukomunisti. Karl Marx na Friedrich Engels walifadhiliwa fedha ili waandike vitabu vitakavyoweka msingi wa itikadi ya Ukomunisti.

Wakati Marx na Engels wakiandika kuhusu nadharia ya ukomunisti, waashi huru walimwajiri mwanafalsafa Friedrich Wilhelm Nietzsche kuandika nadharia inayopingana na ukomunisti ambayo inaonyesha ubora wa watu wa asili ya Aryan.

Lengo la waashi huru kuwapa kazi waandishi hawa kuandika nadharia mbili kinzani ni kuleta mgogoro miongoni mwa wafuasi wa nadharia hizo, hivyo kuleta vita vitakavyopelekea kuanguka kwa nadharia mojawapo. Pia hiki ndicho kilichotokea kwenye vita kuu ya pili ya dunia.

Pike alitabiri vita kuu ya kwanza ya dunia ambayo alisema ilikuwa ni muhimu ili kuuangusha ufalme uliodumu kwa miaka 3000 wa ukoo wa Romanov kule Urusi ili kuifanya Urusi kuwa ni ngome ya Ukomunisti.

Vita hivi vilitokea mwaka 1914-1918 vikifuatiwa na mapinduzi ya Kikomunisti kule Urusi mnamo Oktoba 1918.

Alitabiri Vita Kuu ya Pili ya Dunia, ambayo alisema lengo lake ilikuwa ni kuongeza nguvu ya Uzayuni wa kisiasa na kuanzisha Dola ya Israeli kule Palestina na kuufanya Ukomunisti uwe na nguvu zaidi ya Ukristo. Vita hivi vimetokea kama lilivyotabiriwa.

Vita kuu ya tatu ya dunia ilitabiriwa kuwa ingetokea kutokana na sintofahamu zilizopo kati ya uzayuni wa kisiasa na ulimwengu wa Kiislamu lengo likiwa upande mmoja kuuharibu mwingine.

Vita hivi bado havijatokea japo ishara za kuzuka kwake zipo bayana ukiangalia yanayotokea sehemu mbalimbali za dunia hususan kule Mashariki ya Kati na namna mataifa makubwa yanavyofanya dhuluma mbalimbali dhidi ya mataifa madogo ikiwemo unyonyaji wa rasilimali zao,
- Mwananchi

Post a Comment

أحدث أقدم