Dar Es Salaam.Wakati Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) ikisisitiza
kuwa ratiba ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura itaenda
kama ilivyopangwa, kamati kuu ya chama cha Demokrasi na Maendeleo
imesema itachukua maamuzi magumu endapo shughuli za uboreshaji huo
zitachelewa na kuharibu mchakato wa kura ya maoni.
Mkurugenzi wa NEC, Julius Malaba alisema leo kuwa
uboreshaji utaanza Februari 16 kama ilivyotangazwa awali na utamalizika
kwa wakati ili kupisha ratiba ya kura ya maoni.
“Ratiba inazingatiwa, vifaa vitafika kwa wakati na kuanza kazi kwa wakati,” alisema Malaba.
Akizungumza wakati wa kikao cha dharura cha Kamati
Kuu ya Chadema, Afisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene amesema chama
hicho kimeitisha kikao hicho ili kujadili hatma ya uboreshaji wa daftari
hilo na muda uliobaki kabla ya kupiga kura ya maoni Aprili 30, mwaka
huu.
Pia Chadema walisema kuwa watachukua hatua zaidi
iwapo mashine za Biometric Voters Registration(BVR) zitabainika kuwa na
kasoro katika uboreshaji huo.
Zoezi la kuandikisha Watanzania milioni 26 wenye
sifa ya kupiga kura lilitakiwa kuanza mwezi huu lakini Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (Nec) imesema zoezi hilo litaanza Februari 16, mwaka huu kwa
sababu bado inasubiri mashine 7,750 za (BVR) kwa ajili ya kazi hiyo.
“Kwa mazingira ya kawaida muda uliobaki kwa ajili
ya kazi hiyo kubwa hautoshi ndiyo maana kuitishwa kwa kikao cha dharura
ili kufanya uamuzi,”alisema Makene
إرسال تعليق