Mwanamke nchini Marekani anashikiliwa kwa tuhuma za mauaji baada ya
kuamua kumweka mtoto wake aliyetoka kujifungua katikati ya barabara
kisha kumchoma moto.
Mwendesha mashtaka aliyekua akisimamia kesi hiyo alisema mwanamke huyo Hyphernkemberly Dorvilier anashtakiwa kwa kosa la kuua kwa kukusudia.
Polisi walipofika eneo la tukio walimkuta mtoto huyo akiteketea kwa
moto katikati ya barabara ya makazi ya watu ambayo ni maili 30 kutoka
jiji la Mashariki mwa mji wa Philadelpia na kumkimbiza katika hospitali ya St. Christopher lakini alifariki masaa mawili baada ya tukio hilo.
Mashahidi walisema walimwona mama huyo akichoma kitu lakini hawakujua ni nini na walipomuuliza alisema alikuwa akichoma uchafu.
إرسال تعليق