Msanii maarufu wa muziki wa injili, Rose Muhando.
JE, Rose Muhando nini nani hasa? Hilo ni swali ambalo watu wengi
wanaweza kujiuliza. Yafuatayo ni mambo kadhaa yanayohusiana na nyota
huyo mzaliwa wa Tanzania anayeng’ara katika uimbaji wa nyimbo za Injili
kwa lugha ya Kiswahili katika Afrika ya Mashariki.Mwanamke huyo alizaliwa mwaka 1976 katika kijiji cha Dumila, Wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro akiwa mfuasi wa dini ya Kiislam. Hata hivyo, akiwa na umri wa miaka tisa, akiwa amelala kitandani kwa kulemewa na ugonjwa, alidai kutokewa na Yesu Kristo. Ni baada ya maono hayo ambapo alipona na kuamua kubadili dini kutoka Uislam kwenda Ukristo.
Yafuatayo ni mambo 14 ambayo unahitaji kuyafahamu kuhusu Rose Muhando.
1. Rose Muhando alizaliwa nchini Tanzania, na kukulia mkoani Morogoro.
2. Akiwa msichana, Rose Muhando alihudhuria madrasa ambako alikuwa akipata mafunzo ya dini ya Kiislam baada ya masomo ya kawaida shuleni.
3. Akiwa bado mdogo alikumbwa na ugonjwa wa ajabu ambao ulimlaza kitandani kwa miaka mitatu.
4. Ulikuwa ni wakati akiwa mgonjwa kitandani ambapo Rose Muhando anadai alitokewa na Yesu Kristo ambaye alimponya.
5. Kwa mujibu wa ushuhuda wake, kuna sauti ilimwambia: “Mimi ni Yesu, nimekuponya, hivyo amka unitumikie” na kweli akapona kimiujiza. Baadaye akabadili dini kutoka Uislam na kuwa Mkristo.
6. Ni katika sikukuu moja ya Pasaka ndipo alipobadili dini na kuwa Mkristo.
7. Alianza uimbaji akiwa kiongozi wa kwaya ya Saint Mary ya mjini Dodoma.
8. Alifukuzwa katika kanisa hilo baada ya kukataa matakwa ya kanisa hilo ashiriki katika kurekodi nyimbo na kwaya ya kanisa hilo.
9. Hajaolewa lakini ana watoto watatu wenye umri kati ya miaka tisa na 14.
10. Rose Muhando ameapa hataolewa akisema lengo lake ni kumtumikia Mungu.
11. Mwaka 2009, Rose Muhando alishinda Tuzo ya Mwimbaji Bora Zaidi wa Nyimbo za Injili Tanzania, na alishinda pia Tuzo ya Mwimbaji Bora Zaidi Tanzania na kuzawadiwa Sh. 200, 000 na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kwa kupitia wimbo wake wa ‘Nibebe’
12. Awali, Januari 31, 2005, Rose Muhando alitunukiwa tuzo za Mtunzi Bora Zaidi, Mwimbaji Bora Zaidi na Albam Bora Zaidi ya Mwaka wakati wa Tamasha la Muziki wa Injili Tanzania 2004.
13. Mnamo Februari 2011, Rose Muhando alisaini mkataba wa kurekodi albam na kampuni la Sony Music ambapo hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam Tanzania, tarehe 9 Februari, mkataba ambao ulikuwa wa kwanza wa aina hiyo katika Afrika Mashariki.
14. Mwaka 2008 alipata Tuzo ya Mwimbaji Bora Zaidi wa Nyimbo za Injili Afrika zilizotolewa na Kenya Groove Awards.
Post a Comment