Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, amechaguliwa kuwa Mwenyekiti
mpya wa umoja wa Afrika Au kwenye mkutano unaoendelea mjini Addis Ababa
Ethiopia
Wajumbe walimteuwa Rais Mugabe mwenye umri wa
miaka tisini kwa kauli moja katika mkutano huo na kumtakia mema kwenye
harakati mbalimbali za kuimarisha uchumi wa bara la Afrika.
Mugabe amechukua nafasi hiyo ya Uenyekiti kuziba nafasi inayoachwa na Rais wa Afrika Kusini Nkosazana Dlamini-Zuma.
Wadadisi wa masuala ya kisiasa wametilia shaka
uteuzi huo waRais Mugabe kuongoza Zaidi ya nchi arobaini ambazi ni
wanachama wa umoja huo wakieleza kuwa Mwenyekiti huyo mpya hana
mahusiano mazuri mataifa ya Magharibi
Shaka hiyo dhidi ya Mugabe pia imejadiliwa na
wanasiasa kuwa pengine ikiwa chachu ya maendeleo kwa Afrika kwa
kujitawala yenyewe bila kutegemea nchi wafadhili
إرسال تعليق