Dodoma. Serikali imeunda kikosi kazi kinachoratibiwa na Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) na kujumuisha Mamlaka ya bandari na vyombo vya
ulinzi na usalama ili kudhibiti sukari inayoingia kwa njia za bandari
zisizo rasmi.
Hayo yalisemwa bungeni mjini Dodoma jana na Naibu
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Godfrey Zambi wakati akitoa kauli
ya mawaziri kuhusiana na suala hilo.
Amesema katika kuthibiti sukari inayoingizwa
nchini, serikali imechukua hatua mbalimbali ikiwemo kuunda kamati maalum
ya makatibu wakuu wa wizara za kisekta.
Amesema kamati hiyo iligundua sukari inayoingizwa
sokoni kinyume cha sheria ina sura tatu ikiwemo sukari inayopitia nchi
jirani ambayo haifikishwi kwenye nchi iliyokusudiwa na badala yake
kuuzwa nchini.
Pia sura nyingine ni sukari inayoagizwa kwa
matumizi ya viwandani lakini inauzwa madukani kama sukari ya kawaida na
ile inayoingia nchini kupitia njia zisizo rasmi (bandari bubu).
Amesema katika kukabiliana na changamoto hizo
serikali imeunda kikosi hicho kwa ajili ya kusimamia udhibiti wa sukari
inayopitia nchini kwenda nchi jirani
إرسال تعليق