Kamishana
wa Polisi Oparesheni na Mafunzo, Paulo Chagonja, katika picha hii ya
maktaba akizungumzia tukio la uvamizi wa kituo cha Polisi Ushirombo.
--
Watu wanaosadikika kuwa ni majambazi
yamevamia kituo cha Polisi cha Ikwiriri, Rufiji mkoani Pwani na kuua
Askari wawili na kupora silaha (bunduki) zilizokuwepo kituoni hapo.
Tukio
hilo limetokea usiku wa kuamkia leo,huku askari wanaodaiwa kupotenza
maisha ni Cop. Edgar aliyekatwa mapanga na Wp Judith aliyepigwa risasi
ubavuni upande wa kulia na kutokea upande wa kushoto.
Hivi
sasa hali ni tete katika eneo hilo na watu wamekusanyika huku polisi
wakiongeza nguvu kusaka wauaji katika Tukio la uvamizi, kituo cha polisi
Ikwiriri, Rufiji, Pwani
Hili
ni tukio la tatu katika kipindi cha miezi saba kwa majambazi kuvamia
kituo cha polisi. Juni 11 204, mwaka huu askari polisi mmoja aliuawa baada
ya watu wasiojulikana kuvamia Kituo Kidogo cha Polisi cha Kimanzichana
mkoani Pwani kisha kupora bunduki tatu aina ya SMG na risasi zake.
Usiku
wa Septemba 6, 2014 Askari
wa wawili wa Jeshi la Polisi kituo Kikuu cha Ushirombo kilichopo Wilaya
ya Bukombe mkoani Geita walifariki huku wengine wawili wakijeruhiwa
baada ya kundi la majambazi kuvamia kituo hicho na Aidha katika tukio
hilo, majambazi hayo yalifanikiwa kuchukua baadhi ya silaha zilizopo
kituoni hapo.
إرسال تعليق