Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),
Abdulrahman Kinana, amewaagiza viongozi wa chama hicho kujenga tabia ya
uadilifu katika kutekeleza majukumu yao ya kazi.
Aliyasema hayo wakati akizungumza na wanachama wa CCM katika ziara yake ya kichama mkoa wa Magharibi.
Alisema sifa kubwa ya kiongozi bora ni yule ambaye anawajibika ipasavyo, ikiwamo unapotokea ubadhilifu wakati wa kutekeleza majukumu yake ya kazi bila ya kujali nafasi yake.
Aidha alisema viongozi wa CCM wanatakiwa kufahamu nafasi ya uongozi inakwenda sambamba na maadili, hivyo suala la kuwajibika katika kazi ni lazima. “Kama kiongozi umeshafanya ubadhirifu au umefanya madudu katika uongozi wako usione tabu kujiuzulu endapo utahitajika kufanya hivyo na usisubiri kushurutishwa,” alisema Kinana.
Alisema anakerwa na tabia ya viongozi wabadhirifu na ufisadi huku wakitamba kwa kusema kuwa hawang’oki katika nyazifa walizokabidhiwa kama dhamana.
Katibu Mkuu huyo alisema, kitendo cha kiongozi kujiuzulu mwenyewe bila ya kung’ang’aniwa ni kitendo cha ungwana na kinajenga uaminifu miongoni mwa wananchi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, alisema CCM imejipanga vizuri kuhakikisha majimbo mawili na wadi moja katika Wilaya Magharibi ya Mtoni, Magogoni na wadi ya Tomondo yanarudishwa kutoka upinzani

إرسال تعليق