BARCLEONA YACHANJA MBUGA LA LIGA, YAIBABUA VILLARREAL 3-2 - Neymar, Messi kama kawa


Barcelona inazidi kuifukuza Real Madrid baada ya kuifunga Villarreal 3-2 kwenye mchezo mkali wa La Liga uliochezwa Nou Camp.
Hata hivyo Barcelona walilazimika kutoka nyuma mara mbili kabla ya Lionel Messi hajafunga bao la ushindi dakika ya 55.
Denis Cheryshev aliifungia Villarreal bao la kwanza dakika ya 30, Neymar akachomoa dakika ya 45 kabla ya Villarreal kuwa mbele tena kwa bao la Luciano Dario Vietto dakika ya 52.
Furaha ya Villarreal ilidumu kwa dakika moja tu kabla ya Rafinha hajaisawazishia Barcelona dakika ya 53 na dakika mbili baadae Messi akahitimisha ushindi.
BARCELONA (4-3-3): Bravo; Pique, Mascherano, Alba, Alves; Busquets (Mathieu 72), Iniesta, Rafinha (Rakitic 88); Suarez (Pedro 79), Messi, Neymar  

VILLARREAL (4-4-2): Asenjo; Gaspar, Musacchio, Ruiz, Costa; Pina (Trigueros 77), J Dos Santos (Gomez 85), Cheryshev, Soriano, Vietto, G Dos Santos (Uche 89)

Post a Comment

Previous Post Next Post