Wallpaper zinavyotumika kurembesha kuta

Wengi tumezoea kurembesha kuta za nyumba zetu kwa kutumia rangi lakini kadiri teknolojia inavyokuwa nakshi za urembo nazo zinabadilika na kuja kwa mtindo mwingine.
Unaweza kupigwa na butwaa mara tu uingiapo kwenye nyumba na kukuta ukuta ukiwa unang’ara kwa nakshi za maua.
Kwa haraka haraka unaweza kuhisi rangi zimetumika kuchora ukutani la hasha huo ni mtindo mpya wa kuremba kuta kwa kutumia nakshi maalum zinazofahamika kama ‘wallpapers’.
Nakshi hizi ambazo kwa kiasi fulani zinafanana na kapeti lakini zimekiwa zimetengenezwa maaulum kwa ajili ya kubandikwa ukutani.
Emmanuel Wilbard ambaye ni mwanzishi na mmiliki wa kampuni ya Tanzania Wallpapers Suppliers and Fittings anaeleza kuwa tofauti na rangi nakshi hizo hudumu kwenye ukuta kwa muda wa miaka 10.
Wilbard anaeleza kuwa nakshi hizo kubandikwa kwa kutumia gundi maalum na huweza kuondolewa bila kuharibu ukuta kwa namna yoyote ile.
Anafafanua kuwa kutokana na malighafi iliyotumika kutengeneza nakshi hizo zinaweza kusafishika kwa urahisi kwa kutumia maji.
“Ni teknolojia mpya kwa hapa nchini lakini inaonekana kupokelewa vizuri na watanzania kutokana na namna ilivyo na matokeo mazuri”
“Wallpaper inaweza kubandikwa kwenye kuta za sebuleni,chumbani,jikoni,chooni hata maofisini na kuleta muonekano tofauti”
Ushauri:Tembelea kwenye ukurasa wa Instagram
Wallpaperstz, wallpapersdecoration
Imeandaliwa na Elizabeth Edward

Post a Comment

Previous Post Next Post