Hatimaye Wilfried
Bony ameondoa ukame wake wa magoli kwenye michuano ya kombe la mataifa
ya Afrika (AFCON) baada ya kuifungia Ivory Coast mabao mawili katika
ushindi wa 3-1 dhidi ya Algeria.
Kabla
ya hapo, Bony aliyesajiliwa na Manchester City hivi karibuni na kuwa
mchezaji ghali zaidi Afrika, alikuwa hajafunga hata goli moja kwenye
michuano hii.
Mshambuliaji
huyo alifunga bao la kwanza dakika ya 24 lakini El Arabi Soudani
akaisawazishia Algeria mwanzoni tu mwa kipindi cha pili.
Wilfried
Bony akaongeza bao la pili baada ya kuunganisha free-kick ya Yaya Toure
kabla ya Gervinho kufunga la tatu katika dakika za majeruhi.
Ivory Coast: Gbohouo, Aurier, Bailly, Toure, Kanon, Tiene (Diomande 67), Gradel, Toure, Serey Die, Gervinho, Bony (Tallo 90)
Algeria: M'Bolhi,
Mandi, Bougherra, Medjani, Ghoulam, Taïder, Bentaleb, Feghouli,
Brahimi, Mahrez (Slimani 72 mins), Soudani (Belfodil 72)
Post a Comment