Dar es Salaam. Waziri wa zamani wa Nishati na
Madini, Sospeter Muhongo amekabidhi ofisi kwa Waziri wa sasa, George
Simbachawene katika hafla fupi iliyofanyika ofisini kwake na kumwambia
awe makini katika utendaji kazi hasa kwenye mikataba.
Akikabidhi ofisi, Profesa Muhongo alionya kuhusu
matumizi mabaya ya Ofisi yanayoambata na rushwa ili kuwasaidia
Watanzania masikini wanaoitegemea sekta hiyo kwa maendeleo ya uchumi
wao.
Profesa Muhongo amemuasa Simbachawene kuhusu
umakini na kufanya kazi kwa kuzingatia mikataba inayoweza kuwanuifaisha
Watanzania na rasilimali zao. Simbachawene atasimamia ofisi hiyo kwa
miezi sita kabla ya kuvunjwa kwa bunge baadaye Julai.
Hata hivyo, Profesa Muhongo alimsifu Simbachawene
kuwa hakuwahi kuonyesha ubinafsi wala tamaa na muda wote alikuwa
akizungumzia kuhusu kuwatumikia Watanzania alipokuwa Naibu Waziri wa
wizara hiyo, kwahiyo ana imani naye.
Alisema Tanzania ni lazima ilenge katika kujenga
uchumi imara kupitia sekta ya nishati na madini inayokua kwa kasi ili
Watanzania pia wakue kiuchumi.
Kwa upande wake, Simbachawene alisema ataendeleza
mazuri yaliyoachwa na mtangulizi wake kwa kuweka uwazi kwa kila kitu
kinachofanyika, kwani ofisi ya umma si mali ya mtu
Post a Comment