Morogoro. Shahidi watatu katika kesi inayomkabili Kiongozi wa
jumuiya na taasisi za kiislamu nchini Sheikh Ponda Issa Ponda ametoa
ushahidi wake katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Morogoro huku
mawakili wa upande wa mashtaka na upande wa utetezi wakisigana kwenye
kifungu cha 150 hadi 152 cha sheria ya ushahidi.
Pande hizo mbili zilivutana katika kifungu hicho
baada ya Wakili wa Upande wa utetezi Abubakar Salim kuiomba mahakama
kutoa maamuzi kwa kile alichodai kuwa Wakili wa upande wa mashataka
unamuuliza shahidi maswali ya muongozo kupitia maelezo ambayo yalitolewa
na shahidi aliyepita bila ya kuiomba ruksa mahakama.
Mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo
Mary Moyo, shahidi huyo ambaye ni askari polisi mwenye namba F4103 PC
Ernest anayefanyakazi kwenye chumba cha mashtaka katika kituo kikubwa
cha Polisi mkoa wa Morogoro aliieleza mahakama kuwa Agosti 10 alipokea
maelezo kutoka kwa aliyekuwa Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai mkoa
wa Morogoro Rco Jafert Kibona yanayohusu kesi ya uchochozi inayomkabili
Sheikh Ponda.
Akiongozwa na wakili wa Serikali George Mbalasa
shahidi huyo alieleza kuwa baadaye alifungua kesi yenye namba
RB/8684/2013 na IR/4473/2014 kisha alichukua maelezo mafupi
yaliyoandikwa na Rco ambaye alikuwa kama mlalamikaji kisha kuyaweka
kwenye jarada la kesi hiyo.
Wakili Juma Nassoro wa upande wa utetezi
alimuuliza maswali shahidi huyo ili kutaka kujua kama alikuwepo eneo la
tukio hata hivyo shahidi huyo alidai hakuwepo eneo la tukio bali
alifungua kesi baada ya kupata maelezo kutoka kwa mkubwa wake wa kazi
ambaye ni Rco.
“Mbali na Rco je nani mweingine alikuja kufungua
kesi ama kulalamika kuhusu kesi inayomkabili Sheikh Ponda, na je
ushahidi anaoutoa unauhusiano gani na ushahidi uliotolewa na mashahidi
wengine waliopita katika kesi hiyo” aliuliza Wakili Nassoro.
إرسال تعليق