Waziri
wa Uchukuzi, Samuel Sitta, ametangaza kuwashughulikia watu wote
waliohusika kulihujumu Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), ambalo
'limekufa', huku akionyesha masikitiko yake kuona mpaka sasa hatua kali
hazijachukuliwa dhidi yao.
Sitta alisema hayo, wakati akijibu hoja za wabunge, waliochangia mjadala kuhusu taarifa za kazi za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu na ya Nishati na Madini, kuanzia Januari 2014 hadi Januari 2015, zilizowasilishwa bungeni jana.
Alisema makosa yaliyotendeka huko nyuma dhidi ya ATCL, ni ya ovyo ovyo kabisa na kushauri Bunge liweke utaratibu wa kutunga sheria za kuwabana watu wanaoyatenda.
Sitta alisema hali mbaya iliyopo ATCL inayotokana na deni linaloikabili, inachangiwa kwa kiasi kikubwa na uzembe unaokaribiana na hujuma.
"Sina hakika kama wahusika wamepatiwa dawa yao. Si ajabu wanatamba tu, wako mahali fulani tu wanaangalia. Basi kuna udhaifu fulani lazima tuurekebishe ili tuweze kwenda vizuri," alisema Sitta.
Kuhusu usafiri wa treni ya Dar es Salaam, maarufu kama "Treni ya Mwakyembe", alisema baada ya mkutano kati ya wizara na Wajerumani unaotarajia kufanyika jijini humo, Jumanne ijayo, itaboreshwa zaidi ya ilivyo hivi sasa.
"Kama kawaida yangu mimi ni wa viwango na kasi, mtashangaa hayo yanayokuja katika siku zinazokuja," alisema Sitta.
Alisema kabla ya Rais Jakaya Kikwete hajamaliza kipindi chake cha uongozi, ujenzi wa reli ya kati unaogharimu Sh. Dola za Marekani bilioni 7.6 (Sh. trilioni 11), utakuwa umeanza.
Sitta alisema ni vigumu kiasi hicho cha fedha kupatikana kwenye hazina nchini, hivyo akasema ni lazima sekta binafsi zishirikishwe.
Pia alisema serikali inasubiri kupata mzabuni stahiki ili kuipanua bandari ya Dar es Salaam.
Alisema Dk. Mwakyembe ameweka msingi mzuri wa utendaji kazi katika wizara hiyo, ikiwamo kurudisha maadili pale palipokuwa ovyo, hivyo akaahidi kuendeleza kwa nguvu zote ili taasisi wanazosimamia ziendelee kupata heshima kutokana na majukumu makubwa yanayozikabili.
Sitta amerithi 'mikoba' ya aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Dk. Mwakyembe, aliyehamishiwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki iliyokuwa ikiongozwa naye (Sitta).
Awali, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Peter Serukamba, akiwasilisha taarifa ya kamati yake, alisema kamati imekuwa ikiishauri serikali mara mara kuhusu kuiimarisha ATCL, lakini bado haijaonyesha nia thabiti ya kuifufua.
Hivyo, akasema kama kweli bado serikali inalihitaji shirika hilo la umma, ni lazima itoe mtaji wa kutosha ili kulipa madeni yake yote hatimaye kuifufua upya.
Alisema wawekezaji wamekuwa wakisita kuwekeza ATCL kwa sababu ya madeni ambayo shirika hilo linadaiwa.
"Aidha, kama inasisitiza ushauri wake kuwa biashara hii inahitaji weledi, ujasiri, utashi, uamuzi na kuacha kuchanganya biashara na siasa," alisema Serukamba.
Katika hatua nyingine, Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Martha Mlata, akichangia mjadala huo bungeni jana, alisema Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) linakabiliwa na mtafaruku mkubwa unaohusiana na ajira.
Alisema hali hiyo imekuwa mbaya, kiasi ambacho nafasi husika ya kazi inaweza kutangazwa wakati bado kuna mtu anaishika.
Kutokana na hali hiyo, alishauri kuwapo na utaratibu wa kutangaza ajira katika shirika hilo pale zinapohitajika.
Hata hivyo, alisema kuna vijana wengi wa Kitanzania wana elimu za kuwawezesha kushika nafasi hizo, lakini wanaoajiriwa ni ‘diaspora’ kuzishika katika shirika hilo.

CHANZO:
NIPASHE JUMAPILI
إرسال تعليق