YANGA WATIMULIWA VYUMBANI NA POLISI BAADA YA MECHI YA NDANDA

YANGA jana walilazimika kuondolewa kwenye vyumba vya kubadilisha nguo na polisi, mara baada ya mchezo wao dhidi ya Ndanda kumalizika.


Yanga walitoka suluhu na Ndanda kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, hali iliyowafanya wawe na maongezi marefu vyumbani.

Championi Jumatatu ambalo lilikuwa uwanjani hapo, lilishuhudia baadhi ya polisi waliokuwa kwenye mlango wa kuingilia kwenye vyumba wakibishana na baadhi ya viongozi wa timu hiyo ya Jangwani ambao walikuwa hawataki wachezaji wao watoke.

“Ukweli ni kwamba Yanga hawafanyi sawa, hawaruhusiwi kukaa kwenye vyumba zaidi ya dakika kumi na tano baada ya mchezo kumalizika.

“Nafikiri labda wana kikao, lakini wana usalama wanachofanya ni sahihi kwa kuwa wanatakiwa kuhakikisha wanaondoka hapa salama,” alisema kiongozi mmoja wa ulinzi wa uwanja huo aliyekuwa karibu na eneo la tukio.Hata hivyo, pamoja na mabishano hayo wachezaji na viongozi wa Yanga walitoka na kupanda gari lao na kuondoka

Post a Comment

أحدث أقدم