AUAWA KWA GONGO KISA WIMBO WA CHRISTIAN BELA

MTU mmoja aliyefahamika kwa jina la Abdallah Said, mkazi wa Ukonga, Ilala jijini Dar es Salaam, Jumanne iliyopita alifariki dunia baada ya kupigwa kwa gongo na rafiki yake Maulid Kichuri kwa madai kuwa alikataa kumrudishia ‘memori kadi’ yake ya simu iliyokuwa na wimbo wa Mwanamuziki Christian Bella uitwao Nani Kama Mama.
Abdallah Said enzi za uhai wake akiwa sambamba na jamaa yake.
Kwa mujibu wa mmoja wa marafiki wa wawili hao aliyeomba jina lake lisiandikwe gazetini, tukio hilo lilitokea baada ya awali, Maulidi kumuazima Abdallah memori kadi hiyo iliyokuwa na nyimbo kadhaa, lakini alipotaka kurudishiwa, marehemu alikataa licha ya kushawishiwa kwa ahadi ya kupewa shilingi 3,000(elfu tatu).
“Maulid alikuwa anaupenda sana wimbo wa Bella wa Nani Kama Mama, sasa baada ya kumuazima rafiki yake alitaka na yeye apate burudani, lakini Abdallah alipokataa, alichukua gongo lililokuwepo karibu na kumpiga nalo kichwani.
“Watu tuliokuwepo kwenye tukio tulijaribu kumpa msaada, lakini alikuwa tayari ameshafariki dunia,” alisema shuhuda huyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, DCP Mary Nzuki amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo.
“Tukio hilo lipo na mtuhumiwa tunamshikilia wakati uchunguzi unaendelea,” alisema Kamanda Nzuki.
Marehemu alizikwa katika Makaburi ya Kinyerezi jijini Dar es Salaam, Alhamisi iliyopita.

Post a Comment

أحدث أقدم