Hot News: Majina Ya Walimu Waliopangiwa Kufundisha Shule Za Sekondari YAMESITISHWA Kwa Muda Kutokana Na Kasoro Za Kiufundi Zilizojitokeza

Orodha ya wahitimu wa shahada na stashahada waliopangiwa katika halmashauri mbalimbali inafanyiwa marekebisho baada ya kubainika kuwa uongozi wa Chuo Kikuu cha Sebastian Kolowa (Sebastian Kolowa University College-SEKUCO) cha Lushoto uliwasilisha orodha ya wahitimu wapatao 491 wa mwaka 2013 ambao walishaajiriwa badala ya wahitimu wa mwaka 2014.
Kutokana na sababu hiyo, orodha tajwa imesitishwa kwa muda ili kufanyiwa marekebisho na kuwekwa orodha sahihi itakayojumuisha wahitimu wa SEKUCO wa mwaka 2014.

Tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza kutokana na kasoro hiyo.

Imetolewa na;
OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA



Majina Yaliyoondolewa Yapo Hapa

Post a Comment

أحدث أقدم