Zilizopewa Headlines kwenye Magazeti leo April 28..
Iko stor ya mfanyabiashara Farijala Husein kuhukumiwa kifungo cha miaka 15 baada ya kukutwa na hatia, Rais Kikwete ameshtushwa na taarifa za kuhusishwa na mikakati ya kummaliza Mwenyekiti wa IPP Reginald Mengi,
TFDA imetakiwa kukagua supermarket za mikoani, Tume ya Taifa ya
uchaguzi imepokea vifaa vipya vya BVR 1600 kwa ajili ya uchaguzi, na
kuna TABOA imetangaza kufanya mgomo mwingine nchi nzima April 29.
Ipo taarifa ya watu 3 kukamatwa Mbeya wakiwa na kiganja cha mtu mwenye ulemavu wa ngozi, Rais Kikwete
amemtunuku nishani ya ushupavu Askari wa JWTZ aliyepambana na majambazi
na kuna stori pia ya Jukwaa la Wahariri TZ limesema ikiwa Rais atasani
muswada wa kupitisha sheria za takwimu na makosa mtandaoni litakwenda
mahakamani kupinga.
Kulikuwa na mazungumzo na Katibu mkuu wa TABOA, Enea Mrutu ambae amezungumzia mgomo wanaotaka kuufanya nchi nzima kuanzia kesho endapo nauli mpya haitashushwa.
Utamskia pia Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA, Gilliard Ngewe ambae amezungumzia kanuni ya tozo pamoja na ishu ya mgomo uliopangiwa kufanyika April 29.
إرسال تعليق