Meza
kuu katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani. Kutoka
kushoto ni Makamu wa Rais wa Umoja wa Vilabu vya waandishi wa Habari
nchini (UTPC), Jane Mihanji, Mkurugenzi wa Mfuko wa Vyombo vya Habari
Tanzania (TMF), Bw. Ernest Sungura, Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini
Filiberto Sebregondi na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa
nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP),
Alvaro Rodriguez.
- Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza katika maadhimisho ya Uhuru wa habari duniani yaliyofanyika mkoani Morogoro.
- Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Filiberto Sebregondi akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani.
- Meza kuu katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani. Kutoka kushoto ni Makamu wa Rais wa Umoja wa Vilabu vya waandishi wa Habari nchini (UTPC), Jane Mihanji, Mkurugenzi wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF), Bw. Ernest Sungura, Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Filiberto Sebregondi na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez.
- Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalon Kibanda akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani.
- Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Maelezo, Assah Mwambene akizungumza katika maadhimio hayo.
- Kaimu Meneja wa Uhuru FM, Angela Akilimali (kulia) pamoja na wadau wa vyombo vya habari katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa habari duniani.
- Kutoka kushoto ni Mshauri wa Masuala ya Habari Umoja wa Ulaya, Susane Mbise na Mshauri wa Masuala ya Mawasiliano Umoja wa Mataifa (UN), Hoyce Temu wakifuatilia mijadala katika mkutano huo.
- Mwanahabari na Bloga, Maggid Mjengwa akizungumza katika mkutano huo.
- Mkurugenzi wa Jamii Media, Maxence Mello akizungumza.
- Meza kuu katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani.
Na Joachim Mushi, Morogoro
UMOJA
wa Nchi za Ulaya nchini Tanzania (EU) umepinga vikali vitendo vya
kikatili na unyanyasaji ambavyo wamekuwa wakifanyiwa waandishi wa habari
na vyombo vya dola vya Serikali wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao
ambapo ilitokea mwanahabari mmoja kuuwawa. Alisema hawatachoka kukemea
matukio hayo ya unyanyasaji kwani yanafifisha uhuru wa habari.
Akizungumza
jana mjini Morogoro katika Maadhimisho ya Uhuru wa Vyombo vya Habari
Duniani, Kiongozi Mkuu wa Mabalozi hao, Balozi Filiberto Sebregondi
alisema EU itaendelea kupinga namna yoyote ya unyanyasaji kwa wanahabari
makundi yote wakiwemo wa mitandao ya kijamii hadi utakapo kuwepo uhuru
kamili wa vyombo vya habari.
"...Tulifanya
hivyo kwa mauaji yalipotokea na tutaendelea kufanya hivyo siku zote
watakapo kamatwa na kupigwa wakiwa kazini...Tunajua huenda haitoshi
lakini hii ni kutokana na tofauti mbalimbali za kiutendaji," alisema
Balozi Sebregondi.
Alisema
kupinga unyanyasaji kwa wanahabari haina maana wanachoandika wanahabari
mara zote ni cha kweli lakini ipo namna nzuri ya kushughulikia mvutano
kama huo na kusaidia kupata taarifa za kina zaidi zitakazofikia muafaka.
Aidha
kwa upande wake Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini,
Alvaro Rodriguez ambaye alikuwa mgeni rasmi wa maadhimisho hayo alisema
Tanzania inaongoza Afrika kwa kushindwa kuweka utaratibu mzuri wa
udhibiti mawasiliano.
Alisema
vyombo vya habari ni muhimu katika taifa na hasa kuelekea Uchaguzi Mkuu
wa Taifa unaotarajia kufanyika Oktoba, alisema vyombo vya habari
vinaweza kubomoa au kujenga taifa lolote. "...Waandishi ni watu muhimu
katika kudumisha demokrasia nchini hivyo kuna kila sababu ya kuendelea
kujifunza zaidi.
Maadhimisho
ya uhuru wa vyombo vya habari duniani kitaifa yamefanyika mkoani
Morogoro na kuhudhuriwa na wanahabari mbalimbali, wakongwe, wadau anuai
wa vyombo vya habari huku yakiwa na kauli mbiu ya Usalama wa Vyombo vya
Habari katika Dijitali: Uhandishi Mzuri unaozingatia, Usawa wa Kijinsia
na faragha.
إرسال تعليق